
Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais Balozi Baraka Luvanda akipanda mti kuadhimisha Siku ya Jumuiya ya Nchi za Ukanda wa Bahari ya Hindi (IORA) katika Ofisi za Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mtumba jijini Dodoma.


Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais Balozi Baraka Luvanda (katikati) akiongoza mazoezi ya viungo katika kuadhimisha Siku ya Jumuiya ya Nchi za Ukanda wa Bahari ya Hindi (IORA) katika Ofisi za Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mtumba jijini Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais Balozi Baraka Luvanda akizungumza wakati wa Siku ya Jumuiya ya Nchi za Ukanda wa Bahari ya Hindi (IORA) katika Ofisi za Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mtumba jijini Dodoma.



Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais Balozi Baraka Luvanda akiwa katika maadhimisho ya Siku ya Jumuiya ya Nchi za Ukanda wa Bahari ya Hindi (IORA) katika Ofisi za Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mtumba jijini Dodoma.
======================================================================================
Tanzania imeungana na nchi wanachama wa Jumuiya ya Nchi za Ukanda wa Bahari ya Hindi (IORA) kuadhimisha miaka 29 ya kuanzishwa kwa jumuiya hiyo kwa kupanda miti.
Zoezi la upandaji wa miti lililokwenda sanjari na ufanyaji wa mazoezi mepesi katika Mji wa Serikali Mtumba, Dodoma ni sehemu ya kuhamasisha utunzaji wa mazingira na afya.
Akiongoza maadhimisho hayo, Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais, Balozi Baraka Luvanda alisema IORA inawezesha nchi wanachama kushirikiana katika matumizi endelevu ya rasilimali za Bahari ya Hindi.
Balozi Luvanda ameongeza kuwa nchi hizo wanachama zinawezeshwa pia kukabiliana na changamoto ya uvuvi haramu na kuendeleza uchumi wa buluu katika eneo hilo.
Alisema kuwa zoezi la upandaji miti ni sehemu ya kuunga mkono maono ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia Kampeni ya “27 ya Kijani”.
Halikadhalika, Naibu Katibu Mkuu huyo alisema Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 pamoja na Sera ya Mambo ya Nje ya mwaka 2001 (Toleo la 2024) zinasisitiza uhifadhi wa mazingira.
Maadhimisho ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Nchi za Ukanda wa Bahari ya Hindi yamefanyika chini ya kaulimbiu “IORA Inaboresha Maisha” ikilenga kuongeza uelewa kuhusu umuhimu wa jumuiya hiyo kwa nchi wanachama.