Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu Rasmi ya Ofisi ya Makamu wa Rais

Dkt Muyungi: Sekta binafsi kuchangia 70% ya Dira 2050
Aug 18, 2026
Dkt Muyungi: Sekta binafsi kuchangia 70% ya Dira 2050
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais akizungumza
Na Robert Hokororo

Sekta binafsi nchini inatarajiwa kuchangia takribani asilimia 70 ya utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 iliyozinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Richard Muyungi alipokutana na Ujumbe wa Green Climate Fund (GCF) uliongozwa na Bw. Mihir Sorti, Afisa Mwandamizi eneo la Uwekezaji katika Eneo la Mabadiliko ya Tabianchi jijini Dar es Salaam.

 

Ujumbe wa GCF ulifanya ziara yake nchini Tanzania kuanzia Agosti 11 hadi 14, 2026 na Wadau mbalimbali nchini wa eneo la Fedha za Mabadiliko ya tabianchi mkoani Simiyu na Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa kikao hicho, Dkt. Muyungi alisema kuwa kuna umuhimu mkubwa wa kuimarisha ushiriki wa sekta binafsi katika utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 ambayo imebeba nguzo tatu muhimu.

Pamoja na hayo, Dkt. Muyungi alisisitiza kuwa ushirikiano kati ya Serikali, GCF na sekta binafsi ni muhimu katika kuongeza uwekezaji wa miradi ya kijani, kuchochea ubunifu na matumizi ya teknolojia.

"Ushirikiano wa Serikali na GCF utaongeza upatikanaji wa fedha za tabianchi, hatua zitakazowezesha Tanzania kufikia azma ya kuwa na uchumi wenye pato la Taifa linalofikia Dola za Marekani trilioni moja ifikapo mwaka 2050," alisema Dkt. Muyungi.

Miongoni mwa nguzo tatu zinazounda Dira 2025 ni pamoja na Uchumi Imara, Jumuishi na Shindani ambayo inafungua fursa za kiuchumi na hivyo kuweka mazingira ya kupunguza umaskini na kuboresha hali ya maisha ya wananchi wote. 

Aidha, Nguzo ya pili ni Uwezo wa Watu na Maendeleo ya Jamii ambayo inalenga kuimarisha uwezo wa watu na ustawi wa jamii, ikiwa na dhamira ya dhati katika kuleta usawa wa kijinsia kwa wote na kuwa na jamii jumuishi. Ili kutumia mbinu thabiti zikiambatana na kudumisha maadili mema, kujenga hulka ya kujiamini na kujifunza bila ukomo.

Uchumi imara utahakikisha kwamba maendeleo ya kiuchumi yanawanufaisha wananchi wote na hivyo katika muktadha huu, Tanzania imeendelea kupiga hatua za kiuchumi na kukua kwa wastani wa asilimia 6.2 kwa mwaka katika kipindi cha miongo miwili iliyopita.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi

slot gacor