Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu Rasmi ya Ofisi ya Makamu wa Rais

Balozi Luvanda apokelewa Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Dugange atoa neno
Feb 09, 2026
Balozi Luvanda apokelewa Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Dugange atoa neno
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Festo Dugange akimkaribisha Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. Balozi Baraka Luvanda (kushoto) alipowasili katika Ofisi ya Makamu wa Rais Luthuli jijini Dar es Salaam mara baada ya kuapishwa Ikulu, leo Februari 09, 2026. Katikati ni katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Richard Muyungi.
Na Robert Hokororo

Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. Balozi Baraka Luvanda akiwasili katika Ofisi ya Makamu wa Rais Luthuli jijini Dar es Salaam mara baada ya kuapishwa Ikulu, leo Februari 09, 2026. 

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Richard Muyungi akimkaribisha Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. Balozi Baraka Luvanda (kulia) alipowasili katika Ofisi ya Makamu wa Rais Luthuli jijini Dar es Salaam mara baada ya kuapishwa Ikulu, leo Februari 09, 2026.

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Richard Muyungi akimkaribisha Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. Balozi Baraka Luvanda (kulia) alipowasili katika Ofisi ya Makamu wa Rais Luthuli jijini Dar es Salaam mara baada ya kuapishwa Ikulu, leo Februari 09, 2026. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu (Muungano) Bw. Abdallah Hassan Mitawi.

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Festo Dugange (wa pili kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali akiwemo Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. Balozi Baraka Luvanda (wa pili kulia) alipokaribishwa katika Ofisi ya Makamu wa Rais Luthuli jijini Dar es Salaam mara baada ya kuapishwa Ikulu, leo Februari 09, 2026. Kushoto ni Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Richard Muyungi na Kulia ni Naibu Katibu Mkuu (Muungano) Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Abdallah Hassan Mitawi.

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Festo Dugange (wa pili kushoto) akimpongeza Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. Balozi Baraka Luvanda alipokaribishwa katika Ofisi ya Makamu wa Rais Luthuli jijini Dar es Salaam mara baada ya kuapishwa Ikulu, leo Februari 09, 2026. 

==========================================================================================

Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais Balozi Baraka Luvanda amepokelewa rasmi katika Ofisi za Makamu wa Rais baada ya kuapishwa Ikulu, jijini Dar es Salaam leo Februari 09, 2026. 

 

Hafla hiyo ya mapokezi imefanyika katika Ofisi ndogo ya Makamu wa Rais Luthuli jijini Dar es Salaam na kuongozwa na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muuungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Festo Dugange.

 

Akizungumza awali alipokuwa akimpokea Balozi Luvanda aliyefika ofisini kwake kujitambulisha, Mhe. Dkt. Dugange amemtakia heri Balozi Luvanda katika majukumu yake ya kusimamia Mazingira kwenye Ofisi hiyo.

 

Amesema kuwa yapo mengi katika sekta hiyo muhimu ya mazingira ambayo kwa nafasi yake atakuwa na jukumu la kuyasimamia kuhakikisha mazingira yanakuwa endelevu.

 

Awali, Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Richard Muyungi alimuahidi Balozi Luvanda ushirikiano mkubwa ambao utamuwezesha kufanya shughuli zake kwa ufanisi.

 

Aliwaomba watendaji kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kumpa ushirikiano Balozi Luvanda katika kutekeleza majukumu yake.

 

Alisema Ofisi itaendelea kuimarisha Kituo cha Taifa cha Ufuatiliaji wa Kaboni (NCMC) ili kuhakikisha Serikali inafaidika na biashara ya kaboni kwa kuleta fursa.

 

Kwa upande wake Balozi Luvanda akizungumza na sehemu ya wajumbe wa Menejimenti ya Ofisi ya Makamu wa Rais na Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC), alishukuru kwa mapokezi mazuri aliyoyapata.

 

Alionesha dhamira yake ya kufanya kazi kwa karibu na taasisi zilizo chini ya Ofisi ya Makamu wa Rais, hususan katika masuala ya Muungano na Usimamizi wa Mazingira.

 

Aidha, Naibu Katibu Mkuu huyo alieleza kuwa utekelezaji wa majukumu hayo utaongozwa na maono ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuzingatia Sera, Sheria na Mikakati ya Taifa inayolenga maendeleo endelevu. 

 

Halikadhalika, aliahidi kutumia uzoefu alionao katika kuimarisha usimamizi wa Muungano, kulinda na kuhifadhi mazingira pamoja na kuendeleza ushirikiano kati ya Serikali, taasisi zake na wadau mbalimbali wa maendeleo.

 

Kwa upande mwingine, Balozi Luvanda alihimiza mshikamano na uwajibikaji katika utekelezaji wa majukumu ili kuhakikisha Dira ya Taifa ya Maendeleo (2050) inatekelezwa kwa ufanisi kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho. 

 

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa NEMC, Meneja wa Kanda ya Temeke Bw. Abel Sembeka alimuhakikishia ushirikiano wa karibu kutoka Baraza hilo katika kutekeleza majukumu ya usimamizi na uhifadhi ya mazingira nchini. 

 

Alieleza kuwa NEMC itaendelea kutoa ushauri wa kitaalamu, kusimamia utekelezaji wa sheria za mazingira pamoja na kuimarisha elimu na uhamasishaji wa masuala ya mazingira, sambamba na mwelekeo na vipaumbele vya Ofisi ya Makamu wa Rais.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi