Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu Rasmi ya Ofisi ya Makamu wa Rais

Balozi Mbarouk aipa kongole Ofsi ya Makamu wa Rais kwa kuimarisha Muungano
Aug 04, 2026
Balozi Mbarouk aipa kongole Ofsi ya Makamu wa Rais kwa kuimarisha Muungano
Balozi wa Tanzania Nchini Italia, Mhe. Mbarouk Nassor Mbarouk leo Agosti 4, 2026 Jijini Dodoma wakati akitembelea Banda la Ofisi hiyo katika maonesho ya Kitaifa ya Wakulima na Wafugaji (Nanenane) yanayoendelea katika viwanja vya Dkt. John Malecela.
Na Robert Hokororo

Balozi wa Tanzania Nchini Italia, Mhe. Mbarouk Nassor Mbarouk leo Agosti 4, 2026 Jijini Dodoma wakati alkitembelea Banda la Ofisi hiyo katika maonesho ya Kitaifa ya Wakulima na Wafugaji (Nanenane) yanayoendelea katika viwanja vya Dkt. John Malecela.

Balozi wa Tanzania Nchini Italia, Mhe. Mbarouk Nassor Mbarouk leo Agosti 4, 2026 Jijini Dodoma wakati akisaini kitabu cha wageni alipotembelea Banda la Ofisi hiyo katika maonesho ya Kitaifa ya Wakulima na Wafugaji (Nanenane) yanayoendelea katika viwanja vya Dkt. John Malecela.
 

Balozi wa Tanzania Nchini Italia, Mhe. Mbarouk Nassor Mbarouk leo Agosti 4, 2026 Jijini Dodoma wakati alipotembelea Banda la Ofisi hiyo katika maonesho ya Kitaifa ya Wakulima na Wafugaji (Nanenane) yanayoendelea katika viwanja vya Dkt. John Malecela.
=======================================================================================================

Balozi wa Tanzania Nchini Italia, Mhe. Mbarouk Nassor Mbarouk ameipongeza Ofisi ya Makamu wa Rais kwa juhudi inazoendelea kuchukua katika kuimarisha Muungano.

Mhe. Mbarouk amesema hayo Jumanne Agosti 4, 2026 Jijini Dodoma wakati alipotembelea Banda la Ofisi hiyo katika maonesho ya Kitaifa ya Wakulima na Wafugaji (Nanenane) yanayoendelea katika viwanja vya Dkt. John Malecela.

Balozi Mbarouk amesema hatua hiyo itasadia jamii na Watanzania kufahamu vyema historia, misingi na chimbuko la Muungano na hivyo kuendelea kuenzi misingi ilivyoachwa na waasisi kwa ajili ya mustakabali wa vizazi vya sasa na vijavyo.

Mhe. Mbarouk amesema uwepo wa Muungano umeendelea kuleta manufaa makubwa kwa Watanzania na hivyo kushauri Ofisi ya Makamu wa Rais kuendelea kutoa elimu kwa makundi mbalimbali.

Katika hatua nyingine, Mhe. Mbarouk amepongeza hatua ya kuanzishwa kwa Idara ya Uchumi wa Buluu katika Ofisi ya Makamu wa Rais kwani hatua hiyo itasaidia kuratibu vyema masuala mbalimbali yanayohusu sekta hiyo.

Amesema sekta ya Uchumi wa Buluu ni eneo jipya la kimkakati linaloweza kuongeza wigo wa fursa ya ukuaji wa kipato kwa jamii na hivyo hatua iliyochukuliwa katika kuiweka sekta hiyo ndani ya Ofisi ya Makamu wa Rais itasaidia kuongeza tija.

Awali akitoa maelezo kwa Mhe. Balozi Mbarouk, Afisa Mazingira Mwandamizi Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Abdallah Lungo amesema Ofisi hiyo imeendelea kuimarisha kutoa elimu kwa wananchi na wadau mbalimbali kuhusu masuala ya Muungano Mazingira na Uchumi wa Buluu.

“kwa kutumia nyenzo mbalimbali ikiwemo nyaraka, vitabu, vipeperushi na makala mjongeo kupitia maonesho haya tumeendelea kuwaelimisha wananchi kuhusiana na majukumu yanatekelezwa na Ofisi” amesema Lungo. 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi

slot gacor