












Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni amekutana na kufanya kikao na Wajumbe wa Menejimenti ya Ofisi ya Makamu wa Rais pamoja na viongozi wa taasisi zake (Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) pamoja na Kituo cha Kitaifa cha Kuratibu Kaboni (NCMC).
Kikao hicho kimefanyika Agosti 3, 2026 jijini Dar es Salaam katika Ofisi ya Makamu wa Rais kilihudhuriwa pia na Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. Reuben Kwagilwa, Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Richard Muyungi, Naibu Katibu Mkuu (Muungano) Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Latifa Mohammed Khamis, Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Maduhu Kazi pamoja na viongozi wa Bodi ya Wakurugenzi ya NEMC na NCMC.
Kikao hicho kililenga uboreshwaji wa utekelezaji wa majukumu mbalimbali ya Ofisi ya Makamu wa Rais yanayohusu masuala ya Muungano, Uhifadhi na Utunzaji wa Mazingira pamoja na Uchumi wa Buluu.