


Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Festo Dugange akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Bukoba mkoani Kagera kwa ziara ya kikazi, leo Februari 25, 2026.

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Festo Dugange akipokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Mhe. Erasto Sima wakati akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Bukoba mkoani Kagera kwa ziara ya kikazi, leo Februari 25, 2026.

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Festo Dugange akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Bukoba mkoani Kagera kwa ziara ya kikazi, leo Februari 25, 2026.

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Festo Dugange akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Mhe. Erasto Sima wakati akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Bukoba mkoani Kagera kwa ziara ya kikazi, leo Februari 25, 2025.
===================================================================
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Festo Dugange amewasili leo Februari 25, 2025 katika Uwanja wa Ndege wa Bukoba mkoani Kagera kwa ziara ya kikazi.
Katika uwanja wa ndege huo, Dkt. Dugange amepokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Mhe. Erasto Sima na viongozi mbalimbali.
Katika ziara hiyo Dkt. Dugange, kesho Februari 26, 2026 anatarajiwa kutembelea mradi wa kutenganisha taka ngumu ambao utatekelezwa katika kata ya Kayanga na Mradi wa Vijana wa Kuchakata Taka za Plastiki, Bugene wilayani Karagwe.
Aidha, akiwa katika mradi huo atahamasisha jamii kuhusu usimamizi sahihi wa taka ngumu kwa ajili ya uchakataji na kuelimisha jamii pamoja na kuongeza uratibu wa usimamizi wa taka katika Serikali za Mitaa.
Pia, akiwa wilayani Karagwe, anatarajiwa kutembelea na kukagua mradi wa kutenganisha taka ngumu ambao utatekelezwa katika Kata ya Omurushaka pamoja na mradi wa biashara ya kaboni kupitia kilimo mseto (Kinoni Agroforestry Farm) unaotekelezwa na kampuni ya KADERES.
Huo ni miongoni mwa miradi ambayo inaingiza mapato kwa jamii na Serikali kwa ujumla ambapo katika ziara hiyo atapata uzoefu wa biashara ya kaboni katika kilimo mseto ili kuhamisha biashara hiyo katika ngazi za Mkoa, Wilaya na Halmashauri zinazotekeleza kilimo mseto.
Hivyo, Dkt. Dugange atahitimisha ziara yake kwa kutembelea mradi wa ujenzi wa dampo la maji taka pamoja na eneo kwa ajili ya mradi wa utengenishaji wa taka uliopo wilaya ya Karagwe.