Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu Rasmi ya Ofisi ya Makamu wa Rais

Dkt. Dugange: Uchumi wa Buluu iwe sehemu ya agenda za Vikao vya Muungano
Feb 16, 2026
Dkt. Dugange: Uchumi wa Buluu iwe sehemu ya agenda za Vikao vya Muungano
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Festo Dugange akizungumza wakati wa kikao cha ushirikiano kati ya Ofisi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais kilichoketi Zanzibar leo Februari 16, 2026. Kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais (Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi) Mhe.Hamza Hassan.
Na Robert Hokororo

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Festo Dugange akizungumza wakati wa kikao cha ushirikiano kati ya Ofisi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais kilichoketi Zanzibar leo Februari 16, 2026.Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Festo Dugange ametoa rai kwa watendaji kulipa umuhimu suala la Uchumi wa Buluu katika vikao vya pande mbili za Muungano.

 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais (Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi) Mhe.Hamza Hassan akizungumza wakati wa kikao cha ushirikiano kati ya Ofisi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais kilichoketi Zanzibar leo Februari 16, 2026. Kushoto kwake ni Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Festo Dugange.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais (Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi) Mhe.Hamza Hassan (katikati) akiwa na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Festo Dugange (kushoto kwake) katika picha ya pamoja na wataalamu mara baada ya kikao chaushirikiano kati ya Ofisi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais kilichoketi Zanzibar leo Februari 16, 2026.

============================================================================================================

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Festo Dugange ametoa rai kwa watendaji kulipa umuhimu suala la Uchumi wa Buluu katika vikao vya pande mbili za Muungano.Amesema hayo wakati wa kikao cha ushirikiano kati ya Ofisi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais kilichoketi Zanzibar leo Februari 16, 2026.

Dkt. Dugange amesema kuwa Zanzibar imepiga hatua katika eneo la uchumi hivyo kuendeleza ushirikiano Wake na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutaimarisha uchumi wa Taifa.

Alisema kuwa Ofisi ya Makamu wa Rais tayari imeanzisha Kitengo cha Usimamizi wa Uchumi wa Buluu ambacho ni fursa adhimu kwa wananchi kupata uelewa kuhusu sekta hiyo kupitia elimu inayotolewa.

Aidha, Naibu Waziri alisema kuwa ni muhimu kuzungumzia fursa za Muungano ikiwemo miradi inayotekelezwa katika pande zote mbili badala ya changamoto hivyo kuendelea kujenga imani kwa wananchi.

Pamoja na mambo mengine, aliongeza kuwa Muungano umekuwa ni chachu ya uchumi kwakuwa umeimarisha mazingira kupitia miradi ya maendeleo ikiwemo biashara ya kaboni ambayo inafanyika katika maeneo mbalimbali yakiwemo misitu na hata bahari.

“Tuwapongeze viongozi wetu wa kitaifa yaani Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na Rais Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwa kuimarisha huduma za kijamii na miundombinu, yote hii ni katika kuwanuia wananchi w apande zote mbili za Muungano,” alisema.

Kwa upande Wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais (Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi) Mhe.Hamza Hassan Juma alishauri elimu ya Muungano iendelee kutolewa hususan kwa kundi la vijana.

Alishauri kuwatumia wasanii mbalimbali nchini katika kutoa elimu ya Muungano, kwani wengi wao ni vijana hatua itakayoisaidia kufikisha ujumbe kwa haraka zaidi. 

Halikadhalika, Mhe. Hamza alitoa rai kwa watendaji kutoka Ofisi hizo mbili kutangaza zaidi fursa zinazopatikana katika Muungano badala ya changamoto akisema kuwa Serikali zote zinazishughulikia ili kuzimaliza.

Alipongeza juhudi za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kusimamia sekta ya uchumi ambao umeendelea kuimarika siku hadi siku kwa maendeleo endelevu.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi