Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu Rasmi ya Ofisi ya Makamu wa Rais

Dkt. Muyungi ateta na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Good Neighbors
Jan 23, 2026
Dkt. Muyungi ateta na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Good Neighbors
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Richard Muyungi (kulia) akifanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Good Neighbors Tanzania Bi. Ilsun Jung Dar es Salaam, Januari 23, 2026.
Na Robert Hokororo

====================================================================================================================

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Richard Muyungi (kulia) amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Good Neighbors Tanzania Bi. Ilsun Jung ambao wameonesha nia ya kuwekeza katika Biashara ya Kaboni. Kikao hicho kimefanyika Dar es Salaam, Januari 23, 2026.

Amesema kwamba “Tanzania imekua ikishirikiana na Serikali ya Korea kwa muda mrefu hususani katika sekta ya uhifadhi wa mazingira pamoja na kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi, na hivyo kuipongeza kwa kuendelea kutoa ushirikiano huo”.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi