Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu Rasmi ya Ofisi ya Makamu wa Rais

Makamu wa Rais aeleze mchango wa Marehemu Askofu Shauri
May 06, 2026
Makamu wa Rais aeleze mchango wa Marehemu Askofu Shauri
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akitoa salamu za rambirambi wakati wa Ibada ya Mazishi ya aliyekuwa Askofu wa Pili wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Ruvuma na Katibu Mkuu Mstaafu wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) Marehemu Askofu Stanford Shauri, Ibada iliyofanyika katika Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Ruvuma, Liuli Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma leo tarehe 06 Mei 2026.
Na Robert Hokororo

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akiwasili katika Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Ruvuma kushiriki Ibada ya Mazishi ya aliyekuwa Askofu wa Pili wa Anglikana Dayosisi ya Ruvuma na Katibu Mkuu Mstaafu wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) Marehemu Askofu Stanford Shauri, Ibada inayofanyika Liuli Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma leo tarehe 06 Mei 2026.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akiwasili katika Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Ruvuma kushiriki Ibada ya Mazishi ya aliyekuwa Askofu wa Pili wa Anglikana Dayosisi ya Ruvuma na Katibu Mkuu Mstaafu wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) Marehemu Askofu Stanford Shauri, Ibada inayofanyika Liuli Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma leo tarehe 06 Mei 2026.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akishiriki Ibada ya Mazishi ya aliyekuwa Askofu wa Pili wa Anglikana Dayosisi ya Ruvuma na Katibu Mkuu Mstaafu wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) Marehemu Askofu Stanford Shauri, Ibada inayofanyika Liuli Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma leo tarehe 06 Mei 2026.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akiweka Saini katika kitabu cha maombolezo ya aliyekuwa Askofu wa Pili wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Ruvuma na Katibu Mkuu Mstaafu wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) Marehemu Askofu Stanford Shauri, wakati alipowasili Liuli Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma katika Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Ruvuma kushiriki Ibada ya Mazishi ya Askofu Shauri, leo tarehe 06 Mei 2026.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akiwa na Viongozi mbalimbali wakitazama kuteremshwa kaburini kwa mwili wa aliyekuwa Askofu wa Pili wa  Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Ruvuma na Katibu Mkuu Mstaafu wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) Marehemu Askofu Stanford Shauri, wakati wa  Mazishi yaliyofanyika katika Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Ruvuma, Liuli Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma leo tarehe 06 Mei 2026.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akiweka shada la maua katika kaburi la aliyekuwa Askofu wa Pili wa  Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Ruvuma na Katibu Mkuu Mstaafu wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) Marehemu Askofu Stanford Shauri, wakati wa  Mazishi yaliyofanyika katika Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Ruvuma, Liuli Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma leo tarehe 06 Mei 2026.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akiwa na Viongozi mbalimbali wakisali mbele ya kaburi la aliyekuwa Askofu wa Pili wa  Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Ruvuma na Katibu Mkuu Mstaafu wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) Marehemu Askofu Stanford Shauri, mara baada ya  Mazishi yaliyofanyika katika Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Ruvuma, Liuli Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma leo tarehe 06 Mei 2026.

===============================================================================================================

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mazishi ya aliyekuwa Askofu wa Pili wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Ruvuma na Katibu Mkuu Mstaafu wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) Marehemu Askofu Stanford Shauri.

 

Mazishi hayo yamefanyika katika Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Ruvuma, Liuli Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma.

 

Akitoa salamu za rambirambi kwa niaba ya Rais. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais amesema Serikali inatambua mchango mkubwa aliyoutoa Askofu Shauri katika hapa nchini, akiwa ametumikia Serikali za Mitaa kwa zaidi ya miaka 12 pamoja na kuwa katibu mkuu wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) kwa zaidi ya miaka 10. 

 

Aidha, Makamu wa Rais amesema Marehemu Askofu Shauri amekuwa na mchango mkubwa katika maendeleo ya jamii pamoja na kuendeleza na kuikuza imani ya kikristo nchini.

 

Amesema ni dhamira ya Serikali kuendeleza yale ambayo Marehemu Askofu Shauri aliyasimamia ikiwemo masuala ya amani na haki.

 

Makamu wa Rais amewasilisha salamu za pole kwa familia ya marehemu, Kanisa la Anglikana, wakazi wa Ruvuma, Nyasa na wote walioguswa na msiba huo.

 

Kwa upande wake Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Tanzania Maimbo Mndolwa, ameishukuru Serikali kwa ushirikiano mzuri iliyonayo na Dini katika kutoa huduma mbalimbali kwa wananchi. Ameipongeza Serikali kwa ukarabati wa barabara kutoka Mbambabay hadi Liuli katika Wilaya ya Nyasa ambayo ilikuwa ni changamoto kubwa hali inayodhihirisha kuwajali wananchi wa eneo hilo.

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi

slot gacor