Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu Rasmi ya Ofisi ya Makamu wa Rais

Makamu wa Rais afanya mazungumzo na Mtendaji Mkuu DSE
Feb 13, 2026
Makamu wa Rais afanya mazungumzo na Mtendaji Mkuu DSE
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akifanya mazungumzo na Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) Bw. Peter Nalitolela, mazungumzo yaliyofanyika leo tarehe 13 Februari 2026, Dodoma.
Na Robert Hokororo

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akiwa katika picha ya pamoja na Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) Bw. Peter Nalitolela, mara baada ya mazungumzo mazungumzo yaliyofanyika mkoani Dodoma, leo tarehe 13 Februari 2026. 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akiwa katika picha ya pamoja na Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) Bw. Peter Nalitolela, pamoja na watumishi wa Soko la Hisa la Dar es Salaam na Wasaidizi wa Makamu wa Rais,mara baada ya mazungumzo mazungumzo yaliyofanyika mkoani Dodoma, leo tarehe 13 Februari 2026. 

=====================================================================

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amekutana na kufanya mazungumzo na Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) Bw. Peter Nalitolela, mazungumzo yaliyofanyika leo tarehe 13 Februari 2026, Dodoma.

Katika Mazungumzo hayo, Makamu wa Rais amewahimiza watendaji DSE kuendelea kufanya kazi kwa bidii na kuwa wabunifu katika masuala ya masoko na kuendelea kuvutia uwekezaji.

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) Bw. Peter Nalitolela, ameahidi kuendelea kushirikiana vema na Serikali katika kutafuta mitaji ili kuweza kusaidia utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 ya kufikia uchumi wa Dola za Marekani Trilioni 1 ifikapo 2050.

Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) ni taasisi ya kimkakati ya Taifa inayowezesha ukusanyaji na usimamizi wa mitaji ya muda mrefu kwa ajili ya kufadhili maendeleo ya uchumi wa Tanzania. DSE ni jukwaa rasmi linalowawezesha wawekezaji wa ndani na wa kimataifa kufanya biashara ya hisa, hatifungani, na bidhaa nyingine za kifedha katika mazingira yenye uwazi na utawala bora.

Thamani ya Jumla ya Soko la Hisa la Dar es Salaam ni shilingi Trilioni 31.9, ikiwa na jumla ya wawekezaji waliosajiliwa 779,000

Soko la Hisa la Dar es Salaam ni Mwanachama wa Masoko ya hisa ya Dunia, Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi