Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu Rasmi ya Ofisi ya Makamu wa Rais

Makamu wa Rais awasihi Watanzania kuiombea nchi mwezi huu wa tobą
Mar 11, 2026
Makamu wa Rais awasihi Watanzania kuiombea nchi mwezi huu wa tobą
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akishiriki Iftar aliyoandaa Dodoma, tarehe 11 Machi 2026.
Na Robert Hokororo

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akishiriki Iftar aliyoandaa Dodoma, tarehe 11 Machi 2026. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Balozi Dkt. Asha-Rose Migiro.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akishiriki Iftar aliyoandaa Dodoma, tarehe 11 Machi 2026.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akizungumza aliposhiriki Iftar aliyoandaa Dodoma, tarehe 11 Machi 2026.

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Richard Muyungi akishiriki iftari iliyoandaliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, Dodoma, tarehe 11 Machi 2026.

Naibu Katibu Mkuu (Muungano) Bw. Abdallah Hassan Mitawi akishiriki iftari iliyoandaliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, Dodoma, tarehe 11 Machi 2026.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akiwa katika picha ya pamoja na wananchi na viongozi wa dini wakati akishiriki Iftar aliyoandaa Dodoma, tarehe 11 Machi 2026.

========================================================================

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amewasihi Viongozi wa dini na Watanzania kwa ujumla kutumia mwezi wa toba wa Ramadhani na Kwaresma kuiombea Nchi, Viongozi wa Serikali na Vyama vya Siasa ili kujenga nchi moja yenye upendo na mshikamano.

 

Makamu wa Rais, amesema hayo mara baada ya kushiriki Iftari aliyoiandaa kwaajili ya wananchi mbalimbali wa Mkoa wa Dodoma pamoja na Viongozi wa Serikali, Taasisi za Dini na Chama Cha Mapinduzi, iliyofanyika Mkoani Dodoma.

 

Amesema jambo kubwa ni kuhakikisha hamasa ya mapenzi ya nchi inakuwepo kwa kila mmoja na chemchem ya mapenzi kwa nchi iwepo katika roho ya kila mtanzania ili kuishi kwa kupendana na kushirikiana chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

 

Pia, Makamu wa Rais amesema katika mambo ya maana yanayoweza kufanyakika katika mwezi wa toba ni pamoja na kumuahidi Mwenyezi Mungu kwamba kila mtanzania atafanya jitihada ya kuunganisha watanzania kujenga nchi kuwa nchi moja yenye upendo.

 

Iftar hiyo imehudhuriwa na Viongozi mbalimbali akiwemo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhandishi Hamad Masauni, Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Balozi Dkt. Asha-Rose Migiro, Waziri wa Madini Anthony Mavunde, Kamati ya Maridhiano, Viongozi mbalimbali wa Dini, Wabunge wa Mkoa wa Dodoma, Wakuu wa Wilaya pamoja na wananchi.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi