
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akiwasili katika Ukumbi wa Agape Life Church, uliopo Mbezi Jogoo, Jijini Dar es Salaam, kuwa mgeni rasmi katika hafla ya kusimikwa Uongozi wa Kitaifa wa Awamu ya Tano wa Baraza la Makanisa ya Kipentekoste Tanzania (CPTC), leo tarehe 06 Februari 2026.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akiwasili katika Ukumbi wa Agape Life Church, uliopo Mbezi Jogoo, Jijini Dar es Salaam, kuwa mgeni rasmi katika hafla ya kusimikwa Uongozi wa Kitaifa wa Awamu ya Tano wa Baraza la Makanisa ya Kipentekoste Tanzania (CPTC), leo tarehe 06 Februari 2026.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akishuhudia kuapishwa kwa Mwenyekiti Mpya wa Baraza la Makanisa ya Kipentekoste Tanzania (CPTC), Askofu Dkt. Vernon Fernandes, wakati wa hafla ya kusimikwa Uongozi wa Kitaifa wa Awamu ya Tano wa Baraza la Makanisa ya Kipentekoste Tanzania (CPTC), iliyofanyika katika Ukumbi wa Agape Life Church, uliopo Mbezi Jogoo, Jijini Dar es Salaam leo tarehe 06 Februari 2026.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akiwa na Mwenyekiti wa Baraza la Makanisa ya Kipentekoste Tanzania (CPTC) Askofu Dkt. Vernon Fernandes, wakiungana na Maaskofu na Wachungaji mbalimbali kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati wa hafla ya kusimikwa Uongozi wa Kitaifa wa Awamu ya Tano wa Baraza la Makanisa ya Kipentekoste Tanzania (CPTC), iliyofanyika katika Ukumbi wa Agape Life Church, uliopo Mbezi Jogoo, Jijini Dar es Salaam leo tarehe 06 Februari 2026.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akiwa na Viongozi mbalimbali wa Serikali katika picha ya pamoja na baadhi ya Maaskofu wa Makanisa ya Pentekoste mara baada ya hafla ya kusimikwa Uongozi wa Kitaifa wa Awamu ya Tano wa Baraza la Makanisa ya Kipentekoste Tanzania (CPTC), iliyofanyika katika Ukumbi wa Agape Life Church, uliopo Mbezi Jogoo, Jijini Dar es Salaam leo tarehe 06 Februari 2026.
============================================================================================
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amesema Viongozi wa Dini wana wajibu wa pekee wa kuliombea Taifa kama ambavyo Biblia Takatifu ilivyoelekeza.
Makamu wa Rais ashiriki hafla ya kusimikwa Uongozi wa Kitaifa Makanisa ya Kipentekoste Tanzania (CPTC), iliyofanyika katika Ukumbi wa Agape Life Church, uliopo Mbezi Jogoo, Jijini Dar es Salaam leo tarehe 06 Februari 2026.
Amewahimiza kuendelea kumuombea afya njema, busara na hekima Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwa ndiye kiongozi Mkuu wa Nchi na kupitia yeye nchi itaendelea kuwa salama. Amewataka Viongozi hao kutambua wanapaswa kutimiza wajibu na kuwa na moyo wa utumishi kwa nchi, waumini na Kanisa kwa ujumla.
Halikadhalika, Makamu wa Rais amewahimiza Viongozi wa Dini watambue wajibu wa kulinda mazingira kwa kuendeleza jitihada za uhifadhi mazingira na kuwafundisha waumini kujiepusha na ukataji miti, uchomaji misitu na uharibifu wa vyanzo vya maji. Aidha amewasihi kutoa mafundisho yatakayoichagiza upandaji miti mipya kwa wingi kwa maslahi ya vizazi vya sasa na vijavyo.
Katika hafla hiyo, Makamu wa Rais amesema pamoja na utoaji wa eneo la hekari 12 mkoani Dodoma kwaajili ya ujenzi wa makao makuu ya Baraza la Makanisa ya Kipentekoste Tanzania (CPTC), pia Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa shilingi milioni 100 kwaajili ya kuanzisha ujenzi huo.
Amesema Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan aliunda Wizara maalum kusimamia mahusiano ambayo imeendeleza ushirikiano baina ya Serikali na Taasisi za dini. Ameshukuru Taasisi za dini kwa mchango wanaotoa katika huduma za kijamii kama vile shule na huduma za Afya pamoja na malezi ya watoto
Amewaomba Viongozi hao wa dini kusimamia maadili ya nchi kwa kujenga Taifa la watu wanaoheshimu na wanaojali uwepo wa Mungu. Vilevile kujenga Taifa la watu waaminifu, wanaoheshimiana, wanaopenda nchi, kushirikiana na kuepusha Taifa la watu wabinafsi na wapenda rushwa. Aidha, Makamu wa Rais amesema Serikali itaendelea kusimamia amani ya nchi.