Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu Rasmi ya Ofisi ya Makamu wa Rais

Mhandisi Masauni amtembelea Waziri Mkuu Mstaafu Pinda nyumbani kwake Dodoma Februari 10, 2026.
Feb 10, 2026
Mhandisi Masauni amtembelea Waziri Mkuu Mstaafu Pinda nyumbani kwake Dodoma Februari 10, 2026.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Hamad Yussuf Masauni akimtembelea Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Mizengo Pinda nyumbani kwake Dodoma Februari 10, 2026.
Na Robert Hokororo

==============================================================================================================

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni amemtembelea na kumjulia hali, Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Peter Pinda nyumbani kwake Dodoma, Februari 10, 2026.

Mhandisi Masauni ameeleza nia ya ziara hiyo ni kumjulia hali, kupata uzoefu na ushauri namna bora ya kushughulikia masuala ya Mazingira na Muungano.

Akizungumza, Mhe. Pinda ameshukuru ujio huo na kusa ni hekima na busara kupata mawili matatu kutoka kwa wastaafu. Suala la Mazingira ni suala muhimu sana na ndio maana viongozi wa awamu zote sita wamekuwa wakilitilia maana suala hilo. Hivyo elimu kuhusu masuala ya Muungano na Uhifadhi wa Mazingira inapaswa kutolewa zaidi hasa kwa kundi la vijana ambao wengi wao bado hawana uelewa kwenye mambo hayo.

Aidha Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Pinda ameongezea kuwa ni muhimu Biashara ya Kaboni nayo ikisimamiwa vyema kwani kwa kufanya hivyo itanufaisha jamii na kuongeza pato la taifa endapo watu wataelewa zaidi kuhusu biashara ya kaboni.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi