



Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Richard Muyungi (kulia) akiagana na Mkurugenzi na Mwakilishi wa Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD) nchini Tanzania, Bw. Seth Meng mara baada ya mazungumzo walipokutana katika Ofisi za Makamu wa Rais, Mtumba, Dodoma Mei 5,2026.

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Richard Muyungi (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi na Mwakilishi wa Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD) nchini Tanzania, Bw. Seth Meng na kulia ni Mratibu wa Mpango wa Nchi wa IFAD, Bi. Jacqueline Machangu mara baada ya mazungumzo walipokutana katika Ofisi za Makamu wa Rais, Mtumba, Dodoma Mei 5,2026
==================================================================================================================
Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Richard Muyungi amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi na Mwakilishi wa Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD) nchini Tanzania, Bw. Seth Meng aliyeambatana na Mratibu wa Mpango wa Nchi wa IFAD, Bi. Jacqueline Machangu.
Mazungumzo hayo yamefanyika katika Ofisi za Makamu wa Rais, Mtumba, Dodoma Mei 5,2026 ambapo Kikao kilihusu Mashirikiano kati ya Ofisi ya Makamu wa Rais na IFAD hususan katika utekelezaji wa Miradi ya Mazingira na Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi.
Dkt. Muyungi KM alieleza vipuambele vya Serikali katika hifadhi ya mazingira na uhimilivu wa mabadiliko ya tabianchi kama ilivyobainishwa katika Dira 2050 na Mpango wa Taifa wa Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi (NAP).
Amesema Ofisi ya Makamu wa Rais inakaribisha Wadau kushirikiana na Serikali kutafuta fedha kutoka katika Mifuko Mbalimbali Duniani.
Alisema kuwa OMR itaendelea kutoa mwongozo na kuainisha vipaumbele vya kushirikiana na wadau katika hifadhi ya mazingira, mabadiliko ya tabianchi na Uchumi wa Buluu.
Kwa upande wake, Bw. Meng aliitaja miradi inayotekelezwa nchini na kuwa IFAD iko tayari kuendekea kushirikiana na Ofisi ya Makamu wa Rais kuibua na kutekeleza miradi.