Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu Rasmi ya Ofisi ya Makamu wa Rais

Ofisi ya Makamu wa Rais yaimarisha matumizi ya mifumo ya kidijital
May 05, 2026
Ofisi ya Makamu wa Rais yaimarisha matumizi ya mifumo ya kidijital
Watumishi mbalimbali wa Ofisi ya Makamu wa Rais (OMR) wakifuatilia kwa umakini mafunzo ya TEHAMA yaliyofanyika tarehe 5 Mei 2026 katika Ofisi za OMR, Mtumba, Dodoma.
Na Robert Hokororo

Mkurugenzi wa Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika Ofisi ya Makamu wa Rais, Joyce Mnunguli, ameendesha mafunzo ya kitaalamu kwa watumishi wa OMR yaliyolenga kuimarisha uelewa na matumizi sahihi ya mifumo na programu za TEHAMA katika utoaji wa huduma na utekelezaji wa majukumu ya kila siku. Mafunzo hayo yamefanyika tarehe 5 Mei 2026 katika Ofisi za Makamu wa Rais, Mtumba, Dodoma.

 

Watumishi mbalimbali wa Ofisi ya Makamu wa Rais (OMR) wakifuatilia kwa umakini mafunzo ya TEHAMA yaliyofanyika tarehe 5 Mei 2026 katika Ofisi za OMR, Mtumba, Dodoma. Mafunzo hayo yamelenga kuwawezesha watumishi kuimarisha ufanisi katika matumizi ya mifumo na programu mbalimbali za TEHAMA kwa ajili ya kuboresha utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.

Watumishi mbalimbali wa Ofisi ya Makamu wa Rais (OMR) wakifuatilia kwa umakini mafunzo ya TEHAMA yaliyofanyika tarehe 5 Mei 2026 katika Ofisi za OMR, Mtumba, Dodoma. Mafunzo hayo yamelenga kuwawezesha watumishi kuimarisha ufanisi katika matumizi ya mifumo na programu mbalimbali za TEHAMA kwa ajili ya kuboresha utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.

===================================================================================================================

Mkurugenzi wa Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika Ofisi ya Makamu wa Rais (OMR), Bi. Joyce Mnunguli, ameendesha mafunzo ya kitaalamu kwa watumishi wa ofisi hiyo (E-Barua) yaliyolenga kuimarisha uelewa na matumizi sahihi ya mifumo na programu za TEHAMA katika utoaji wa huduma na utekelezaji wa majukumu ya kila siku.

Mafunzo hayo yaliyofanyika tarehe 5 Mei 2026 katika Ofisi za Makamu wa Rais, Mtumba jijini Dodoma, yamehusisha watumishi kutoka idara na vitengo mbalimbali ndani ya OMR, ambapo walipata fursa ya kujifunza na kuboresha ujuzi wao katika matumizi ya teknolojia za kisasa.

Mada zilizowasilishwa zilijikita katika matumizi bora ya mifumo ya ndani ya ofisi, usalama wa taarifa (information security), pamoja na mbinu za kuongeza ufanisi kwa kutumia programu mbalimbali za kidijitali.

Akizungumza wakati wa mafunzo hayo, Bi. Mnunguli alisisitiza umuhimu wa watumishi kuendana na kasi ya maendeleo ya TEHAMA ili kuongeza tija katika utendaji kazi na kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.

Alibainisha kuwa matumizi sahihi ya mifumo na programu si tu yanarahisisha kazi, bali pia yanasaidia kuongeza uwajibikaji na uwazi katika taasisi za umma.

Kwa upande wao, watumishi wa OMR walifuatilia kwa makini mafunzo hayo na kushiriki kikamilifu kupitia mijadala na maswali mbalimbali, hali iliyoonesha dhamira yao ya kujifunza na kuimarisha utendaji kazi wao.

Ushiriki huo unatarajiwa kuwa chachu ya mabadiliko chanya katika matumizi ya TEHAMA ndani ya ofisi hiyo.
Kwa ujumla, mafunzo hayo ni sehemu ya jitihada za Ofisi ya Makamu wa Rais katika kuhakikisha watumishi wake wanakuwa na ujuzi na uwezo unaohitajika ili kuendana na mageuzi ya kidijitali, kuongeza ufanisi, na kutoa huduma bora zaidi kwa umma.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi