Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu Rasmi ya Ofisi ya Makamu wa Rais

Ofisi ya Makamu wa Rais yawanoa wabunge kuhusu hifadhi ya mazingira
Feb 13, 2026
Ofisi ya Makamu wa Rais yawanoa wabunge kuhusu hifadhi ya mazingira
Wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira wakiwa katika Semina kuhusu Mipango na Mikakati ya Serikali ya Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira iliyotolewa na Ofisi ya Makamu wa Rais jijini Dodoma Februari 13, 2026.
Na Robert Hokororo

 

==================================================================================================

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni amesema Masuala ya mazingira na mabadiliko ya tabianchi kutambuliwa na kupewa umuhimu katika Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 ni mafanikio makubwa katika utekelezaji mipango na mikakati ya Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira.

Amezungumza hayo wakati wa Semina kuhusu Mipango na Mikakati ya Serikali ya Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira iliyotolewa na Ofisi ya Makamu wa Rais kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira jijini Dodoma Februari 13, 2026.

Amesema mafanikio mengine ni pamoja na Uanzishwaji kisheria wa Kituo cha Taifa cha Ufuatiliaji wa Kaboni na Kamati ya Taifa ya Mabadiliko ya Tabianchi pamoja na Kujumuishwa kwa masuala ya mazingira na mabadiliko ya tabianchi katika sera pamoja na mikakati na mipango na bajeti ya Serikali

“Utekelezaji wa Miradi Biashara ya Kaboni nchini na utekelezaji wa mradi wa udhibiti uchafuzi wa mazingira unaotokana na matumizi ya zebaki mikoa ya Geita, Mwanza, Mara, Shinyanga, Singida, Mbeya na Songwe,”

“Ujenzi wa maabara na vitendea kazi kuwezesha ufuatiliaji wa zebaki katika maji, hewa na ardhi maeneo ya waachimbaji wadogo ni mafanikio mengine tuliyopata,” ameeelezea Mhe. Masauni.

Aidha amesema mafanikio mengine ni pamoja na Ujenzi wa vituo (8) vya mfano vya uchenjuaji salama wa dhahabu kwa kutumia zebaki katika mikoa ya (Mwanza, Geita, Singida, Mara, Mbeya, Songwe, na Shinyanga pamoja na ujenzi wa kituo cha kukuza uelewa kwa wachimbaji madini kuhusu masuala ya zebaki Geita.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira Mhe. Jackson Kiswaga amesema suala la uhifadhi wa mazingira na utunzaji halina mipaka hivyo kila mmoja anapaswa kuwajibika kulingana na nafasi yake.

Mhe. Kiswaga amesisitiza suala la elimu kupewa kipaumbele kwa wananchi ili waweze kuelewa namna ya utenganishaji wa taka ikiwa pamoja na kutazama bajeti katika eneo la mazingira kuanzia ngazi ya chini kwa kuwa kila mmoja anatamani kuona mabadiliko kwenye mazingira.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi