
Naibu katibu Mkuu (Mazingira) Balozi Baraka Luvanda (katikati) akiwa na Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Kemilembe Mutasa (kushoto) pamoja na Mkurugenzi Msaidizi wa Mazingira Dkt. Kanizio Manyika wakati wa kikao cha uanzishwaji wa Mradi wa kuimarisha jamii na mifumo ikolojia katika katika kustahimili Athari za Mabadiliko ya Tabianchi kwenye Ukanda wa Misitu ya Miombo Tanzania Bara na kame, Zanzibar kilichofanyika leo Machi 17, 2026 jijini Dodoma.

Naibu katibu Mkuu (Mazingira) Balozi Baraka Luvanda (waliokaa katikati) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa kikao cha uanzishwaji wa Mradi wa kuimarisha jamii na mifumo ikolojia katika katika kustahimili Athari za Mabadiliko ya Tabianchi kwenye Ukanda wa Misitu ya Miombo Tanzania Bara na kame, Zanzibar kilichofanyika leo Machi 17, 2026 jijini Dodoma.
====================================================================
Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais imeanzisha Mradi wa kuimarisha jamii na mifumo ikolojia katika katika kustahimili Athari za Mabadiliko ya Tabianchi kwenye Ukanda wa Misitu ya Miombo Tanzania Bara na kame, Zanzibar wenye thamani ya shilingi bilioni 10.6.Mradi huo unatarajiwa kuanza kutekelezwa katika wilaya ya Sikonge (Tabora), Tanganyika na Nsimbo (Katavi), Nkasi (Rukwa), Kusini Unguja (Mkoa wa Kusini), Kaskazini ‘B’ (Mkoa wa Kaskazini Unguja), Chakechake (Kusini Pemba) na Micheweni) Kaskazini Pemba.Akifungu kikao hicho leo Machi 17, 2026 jijini Dodoma, Naibu katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais Balozi Baraka Luvanda amezitaka taasisi na wadau kufanya kazi kwa ushirikiano, uwazi na kwa njia shirikishi, ili kuendana na mipango ya maendeleo ya ndani na vipaumbele vya jamii. Alieleza kuwa mradi huo unajibu moja kwa moja utekelezaji wa vipaumbele vya kitaifa na lengo kupunguza mazingira magumu na kuongeza ustahimilivu wa hali ya hewa kwa jamii na sekta za kipaumbele kwa kuongeza teknolojia zinazofaa.Kwa mujibu wa Balozi Luvanda, mradi huo utasaidia kuboresha mazingira wezeshi ili kukuza matumizi ya teknolojia ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kupitia sera zilizoimarishwa, taasisi na mifumo ya usaidizi wa maamuzi.Alisema Serikali imechukua hatua za uharibifu wa mazingira kwa kuanzisha sera, mikakati na ahadi za kimataifa, zikiwemo Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, Sera ya Taifa ya Mazingira (2021), Mkakati wa Kitaifa wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (2021-2026), Sheria ya Usimamizi wa Mazingira, Sura ya 191 na Michango Iliyoamuliwa Kitaifa chini ya Mpango Mkakati wa Paris wa 2021. Sanjari na hilo, alibainisha kuwa mradi utasaidia mifumo ya shughuli za kujipatia kipato zikiwemo kilimo kinachozingatia hali ya hewa, uvunaji wa maji, kilimo mseto na huduma za ugani za kidijitali.Halikadhalika, Naibu Katibu Mkuu huyo alisema mradi utakuwa ni hatua mojawapo ya kuchochea matumizi ya teknolojia mbadala wa matumizi ya mazao yasiyo ya mbao ili kupunguza ukataji wa miti.Aidha, Balozi Luvanda alisema mabadiliko ya hali ya hewa yanaendelea kuleta hatari kubwa kwa maisha, usalama wa chakula, mifumo ya ikolojia na maendeleo ya taifa na kuwa misitu ya miombo na nchi kavu za Zanzibar ni ziko hatarini zaidi kuathiriwa.
Awali akitoa maelezo kuhusu kikao hicho cha uanzishwaji wa mradi huo, Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Kemilembe Mutasa alisema wajumbe wa kikao wamejadili kuhusu mpango kazi wa utekelezaji wa mradi na manunuzi.
Alisema tayari tathmini ya walio katika mradi imefanyika na kuonesha kuwa maeneo mengi yanakabiliwa na changamoto mbalimbali za kimazingira na kijamii ikiwemo uharibifu wa misitu.
Bi. Kemi aliongeza kuwa kwa vile washiriki wa kikao hicho ni wataalamu kutoka taasisi mbalimbali za Serikali jukumu lililoko mbele yao ni kutoa ushauri wa kitaalamu kuhusu utekelezaji wa mradi.
Utekelezaji wa mradi huo unaishirikisha Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar pamoja na Wizara zenye dhamana na Kilimo, Umwagiliaji, Malisili na Mifugo kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.