Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu Rasmi ya Ofisi ya Makamu wa Rais

Serikali yatoa kipaumbele masuala ya hifadhi ya mazingira
Feb 18, 2026
Serikali yatoa kipaumbele masuala ya hifadhi ya mazingira
Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Abdallah Hassan Mitawi akizungumza wakati wa kikao cha kamati ya Taifa ya ushauri wa Mabadiliko ya Tabianchi kilichofanyika jijini Dar-es-salaam Februari 18,2026
Na Robert Hokororo

Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais Balozi Baraka Luvanda akitoa neno la ufunguzi wakati wa kikao cha kamati ya Taifa ya ushauri wa Mabadiliko ya Tabianchi kilichofanyika jijini Dar-es-salaam Februari 18, 2026.

Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais, Bi.Kemilembe Mutasa akitoa wasilisho kuhusu Dira ya Maendeleo ya Taifa-2050, na mwelekeo wa Hifadhi ya Mazingira na Ustahimilivu wa Mabadiliko ya Tabianchi wakati wa kikao cha kamati ya Taifa ya ushauri wa Mabadiliko ya Tabianchi kilichofanyika jijini Dar-es-salaam Februari 18, 2026.

Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Dkt. Immaculate Semesi akiwasilisha mada wakati wakati wa kikao cha kamati ya Taifa ya ushauri wa Mabadiliko ya Tabianchi kilichofanyika jijini Dar-es-salaam Februari 18, 2026.

Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Deogratius Paul akitoa wasilisho wakati wa kikao cha kamati ya Taifa ya ushauri wa Mabadiliko ya Tabianchi kilichofanyika jijini Dar-es-salaam Februari 18,2026.

Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma za Sheria Ofisi ya Makamu wa Rais, Bw. Dustan Shimbo akiwasilisha mada wakati wa kikao cha kamati ya Taifa ya ushauri wa Mabadiliko ya Tabianchi kilichofanyika jijini Dar-es-salaam Februari 18,2026.

=============================================================================================

Kamati ya Taifa ya Ushauri kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi na Uhifadhi wa Mazingira imekutana na kujadili vipaumbele vinavyohusu uhifadhi wa mazingira, kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi pamoja na kuimarisha utekelezaji wa sera, mikakati na mipango ya Kitaifa.


Akifungua kikao hicho, Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Abdallah Hassan Mitawi leo Februari 18, 2026 jijini Dar es Salaam amesema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeendelea kutoa kipaumbele kwenye masula ya mazingira kama sehemu ya msingi wa maendeleo endelevu.

Bw. Mitawi alisema kuwa hatua hiyo inaakisiwa katika utekelezaji wa Dira ya Taifa 2050, Sera ya Taifa ya Mazingira ya mwaka 2021, Sheria ya Usimamizi wa Mazingira (Sura ya 191) Pamoja na marekebisho yake, mikakati pamoja na programu na miradi mbalimbali inayolenga kulinda na kuhifadhi rasilimali asilia.

Aliongeza kuwa katika miaka ya hivi karibuni, Serikali imefanya mageuzi makubwa ya kisera na kisheria pamoja na kuendelea kutekeleza miradi mikubwa ya kimkakati katika sekta ya nishati, miundombinu, kilimo, madini, viwanda na Uchumi wa Buluu.

Kutokana na hayo, Bw. Mitawi alisisitiza kuwa mageuzi haya yanahitaji ushauri wa kina wa kitaalamu wa pamoja ili kuhakikisha kuwa mwelekeo wa maendeleo unalinda maslahi ya kizazi cha sasa na kijacho.

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais Balozi Baraka Luvanda alikumbusha kuwa Kifungu cha 11 (1-3) cha Sheria ya Usimazi wa Mazingira sura 191, pamoja na marekebisho yake mwaka 2025, kimeelekeza kuwepo kwa Kamati ya Taifa ya Ushauri wa Mazingira ambayo pia ni Kamati ya uongozi wa Mabadiliko ya Tabianchi.

Alisema kuwa kazi ya Kamati hiyo ni kumshauri Waziri mwenye dhamana ya Mazingira nchini kuhusu masula ya mbalimbali yanayohusu mazingira na kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi