


====================================================================================================
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Qatar Nchini Tanzania Mhe. Fahad Rashid Al-Marekhi, Februari 16, 2026, Jijini Dar ES Salaam. Lengo kuu la ziara hiyo lilikuwa kujadili maeneo ya ushirikiano kati ya Tanzania na Qatar katika suala la Uhifadhi na Utunzaji wa Mazingira.