Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu Rasmi ya Ofisi ya Makamu wa Rais

Dkt Muyungi, BRAC kuimarisha ushirikiano katika hifadhi ya mazingira
Jul 22, 2026
Dkt Muyungi, BRAC kuimarisha ushirikiano katika hifadhi ya mazingira
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Richard Muyingi akifanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu Shirika la BRAC Maendeleo Tanzania Bw. Joydeep Sinha ofisini kwake jijini Dodoma leo Julai 22, 2026 kwa lengo la kuimarisha ushirikiano katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za maendeleo na hifadhi ya mazingira.
Na Robert Hokororo

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Richard Muyingi akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe kutoka Shirika la BRAC Maendeleo Tanzania mara baada ya kufanya mazungumzo ofisini kwake jijini Dodoma leo Julai 22, 2026 kwa lengo la kuimarisha ushirikiano katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za maendeleo na hifadhi ya mazingira.

=============================================================================================================

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Richard Muyingi amekutana na kufanya mazungumzo na ujumbe kutoka Shirika la BRAC Maendeleo Tanzania ofisini kwake jijini Dodoma leo Julai 22, 2026.

Lengo la mazungumzo hayo ni kuimarisha ushirikiano na kudumisha mshikamano katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za maendeleo.

Katika mazungumzo hayo, pande zote mbili zilijadili fursa za kupanua ushirikiano katika utekelezaji wa mradi mpya unaojulikana kama BIGBET—programu ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Programu hiyo inalenga kuwawezesha wanawake kujenga ustahimilivu na kuwaondoa katika mazingira ya hatari yanayosababishwa na mabadiliko ya tabianchi.

Mradi huo unatarajiwa kutekelezwa na BRAC Maendeleo Tanzania kwa ushirikiano na Serikali pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo katika nchi nne, ukiwa na lengo la kuleta matokeo chanya na endelevu kwa jamii zinazolengwa.

Aidha, ujumbe huo uliongozwa na Mkurugenzi Mkuu Bw. Joydeep Sinha, akiambatana na Meneja wa Mradi Bw. Jumanne Magese na Naibu Meneja wa Uhamasishaji wa Rasilimali Kelvin Edward.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi

slot gacor