
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Richard Muyungi (kushoto) akifanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la linalojihusisha na uhifadhi la Frankfurt Zoologist Society (FSZ) la nchini Ujerumani, Dkt. Maurus Msuha, ofisini kwake jijini Dodoma Dodoma leo Julai 22, 2026.

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Richard Muyungi (wa pili kulia) akifanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la linalojihusisha na uhifadhi la Frankfurt Zoologist Society (FSZ) la nchini Ujerumani, Dkt. Maurus Msuha, ofisini kwake jijini Dodoma Dodoma leo Julai 22, 2026.

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Richard Muyungi (kushoto) akiwa na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la linalojihusisha na uhifadhi la Frankfurt Zoologist Society (FSZ) la nchini Ujerumani, Dkt. Maurus Msuha mara baada ya kikao, ofisini kwake jijini Dodoma Dodoma leo Julai 22, 2026.

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Richard Muyungi (kushoto) akiagana na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la linalojihusisha na uhifadhi la Frankfurt Zoologist Society (FSZ) la nchini Ujerumani, Dkt. Maurus Msuha mara baada ya kufanya mazungumzo, ofisini kwake jijini Dodoma Dodoma leo Julai 22, 2026.
=======================================================================================
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Richard Muyungi amesema uhusiano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Ujerumani umeendelea kuimarika hivyo kuchochea ushirikiano katika masuala ya hifadhi ya mazingira.
Amesema hayo alipokutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la linalojihusisha na uhifadhi la Frankfurt Zoologist Society (FSZ) la nchini Ujerumani, Dkt. Maurus Msuha, ofisini kwake jijini Dodoma Dodoma leo Julai 22, 2026.
Dkt. Muyungi alisema kuwa ipo mikataba mbalimbali takriban mitatu ya kimataifa inayohusu usimamizi wa mazingira Tanzania iliingia ambayo kimsingi Tanzania imeendelea kunufaika nayo.
Pia, aliomba Serikali ya nchi hiyo kuendelea kushirikiana na Tanzania katika kuchangia masuala ya mazingira hususan katika kutoa fedha za miradi ya maendeleo ikiwemo katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
“Kama tunavyofahamu, mwaka huu tunaanza utekelezaji wa Dira 205O hivyo tunahakikisha hifadhi ya mazingira ambayo Ofisi ya Makamu wa Rais tunasimamia yanakuwa na mchango katika jamii lakini yote haya yanahitaji fedha,” alisema.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkazi Dkt. Msuha alisema kuwa shirika hilo linaiunga mkono Serikali katika masuala ya uhifadhi wa mazingira kwa kufanya kazi na mashirika yanahusiana na hifadhi ya wanyapori.
Alisema kwa sasa wako katika mpango wa kuboresha maeneo ya hifadjhi na hata nje ya hifadhi kwa kuhusisha wananchi waliopo katika maeneo hayo kushiriki katika kubioresha hifadhi.
Dkt. Msuha aliongeza kuwa kupitia utaratibu huo wameandaa mfumo unaowezesha wananchi kushiriki katika shughuli za kijamii bila kuharibu mfumo ikolojia na kuboresha maisha ya jamii zinazozunguka hifadhi na kuwafanya kutojiingiza katika vitendo vya kijangili.