Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu Rasmi ya Ofisi ya Makamu wa Rais

Makamu wa Rais: Serikali imedhamiria kuhakikisha Katiba mpya inapatikana
Jul 24, 2026
Makamu wa Rais: Serikali imedhamiria kuhakikisha Katiba mpya inapatikana
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akishiriki ufunguzi wa Mkutano wa 15 wa Mwaka wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) uliofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam, leo tarehe 24 Julai 2026.
Na Robert Hokororo

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akiwa na viongozi mbalimbali katika picha ya pamoja na wadau mbalimbali wa haki za binadamu wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 15 wa Mwaka wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) uliofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam, leo tarehe 24 Julai 2026.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akiondoka katika Ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam mara baada ya ufunguzi wa Mkutano wa 15 wa Mwaka wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC). Tarehe 24 Julai 2026.

===============================================================================================

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ana dhamira ya dhati wa kuhakikisha Katiba mpya inapatikana, ndio maana suala hilo limewekwa katika Ilani ya Chama Cha Mapinduzi pamoja na kuahidi kulitekeleza.

Makamu wa Rais amesema hayo wakati akifungua Mkutano wa 15 wa Wanachama wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC) uliyofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City, Jijini Dar es Salaam. Amesema suala hilo limejadiliwa tangu mwaka 1992 mara baada ya kuanza kwa vyama vingi, lakini Serikali ya Awamu ya Sita imeahidi kulitekeleza kwa manufaa ya wananchi.  Amewasihi wananchi kuibeba ajenda hiyo kwa uzito mkubwa ili iweze kutekelezwa katika kipindi hiki.

Aidha, Makamu wa Rais amesema ni muhimu kuzingatia suala la haki, kwani ndio msingi wa amani katika Taifa lolote lile. Amesema Serikali itaendelea na wajibu wa kuhakikisha wananchi wanaishi kwa usalama bila hofu.

Vilevile, Makamu wa Rais amesema ni vema kutambua kwamba si lazima Serikali ikubaliane kila kitu na watetezi wa haki za binadamu kwa kuwa Tanzania ni nchi yenye watu wenye uelewa na mawazo tofauti. Makamu wa Rais amesema Serikali inatambua watetezi wa haki za binadamu ni wadau muhimu katika kutekeleza Dira ya Taifa 2050, kwa kuzingatia jambo lililoelezwa kwa kina katika dira hiyo ni kujenga jamii inayozingatia haki za binadamu kama vile utawala bora, ushirikishwaji wa jamii na usawa

Makamu wa Rais ameongeza kwamba, Serikali itaendelea kuweka mazingira wezeshi ili kuzifanya Taasisi za Haki za Binadamu kufanya kazi zake kwa ufanisi na kuleta tija iliyokusudiwa kwa Taifa. Amesema Serikali itaendelea kuwapa ushirikiano na kuzingatia usalama wa watetezi wa haki za binadamu ili waweze kufanya kazi zao pasi na hofu. 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi

slot gacor