Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu Rasmi ya Ofisi ya Makamu wa Rais

Katibu Mkuu Dkt Muyungi awafunda mabalozi wa mazingira
Jul 22, 2026
Katibu Mkuu Dkt Muyungi awafunda mabalozi wa mazingira
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Richard Muyungi akizungumza wakati wa kikao na mabalozi wa mazingira kilichofanyika Julai 22, 2026 ukumbi wa Ofisi ya Makamu wa Rais jijini Dodoma kwa lengo la kujadili na kuweka mikakati ya usimamizi endelevu wa mazingira.
Na Robert Hokororo

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Richard Muyungi akiwa katika picha ya pamoja na mabalozi wa mazingira mara baada ya kikao kilichofanyika Julai 22, 2026 ukumbi wa Ofisi ya Makamu wa Rais jijini Dodoma kwa lengo la kujadili na kuweka mikakati ya usimamizi endelevu wa mazingira.

.================================================================================================================

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Richard Muyungi amesema mabalozi wa mazingira wana nafasi kubwa katika kuisaidia nchi katika kuimarisha usimamizi wa mazingira.

 

Ametoa kauli hiyo alipokutana na mabalozi wa mazingira katika ukumbi wa Ofisi ya Makamu wa Rais jijini Dodoma kwa lengo la kujadili na kuweka mikakati ya usimamizi endelevu wa mazingira.

 

Akizungumza na mabalozi hao, Dkt. Muyungi pamoja na kuwapongeza kwa kazi nzuri ya kujitoa aliwahimiza kuendelea kuendelea kushirikiana na Serikali katika utekelezaji wa mikatati yake ikiwemo katika utekelezaji wa Dira 2050 hususan upandaji wa miti bilioni 10 ifikapo mwaka 2030.

 

Aliwaomba mabalozi hao wa mazingira waendelee kuhamasisha wananchi katika maeneo yao kushiriki kikamilifu katika zoezi la kukijanisha Tanzania kwa kupanda miti na kuitunza ili kunusuru kuenea kwa jangwa.

“Usimamizi wa vyanzo vya maji katika mabonde yetu ni muhimu ili tupate nishati yote haya hatuwezi bila ninyi mabalozi kushiriki katika kuhamasisha jamii ambayo mko nayo katika maeneo yenu, tuendelee kushirikiana,” alisema Dkt. Muyungi.

 

Aidha, Katibu Mkuu huyo alibainisha kuwa ni asilimia 37 ya taka zote hukusanya na kuchakatwa hivyo ni wakati sasa kwa kushirikiana na mabalozi wa mazingira kuhakikisha usimamizi wa taka unaimarika na kufikisha asilimia 100.

 

Halikadhalika, alieleza kuwa mabalozi wa mazingira wawe chachu ya kuelimisha na kuhamasisha jamii katika matumizi ya nishati safi ya kupikia ambayo Serikali imeweka lengo kuwa ifikapo mwaka 2030 asilimia 80 ya wananchi wawe wanatumia.

 

Kutokana na hali hiyo, Dkt. Muyungi alisema kuwa nishati safi inaongeza utu wa mtanzania na ni jambo la msingi kwani lina mambo makuu ambayo yatabadilisha nchi na kuwa na fikra za kuondokana na ukataji wa miti kwa ajili ya kuni na mkaa hivyo kulinda misitu.

 

“Tunapohimiza nishati safi tunahimiza pia kuondokana na umasikini na uharibifu wa mazingira pamoja na kutoa fursa kenye makundi ya wanawake na wasichana ili waende shule badala ya kutumia muda wao kwenda porini na kukata kuni,“ alisisitiza.

 

Sanjari na hilo alisema katika utunzaji wa mazingira kupitia misitu baada ya upandaji wa miti kuna fursa ya biashara ya kaboni hivyo alitoa rai kwa mabalozi wa mazingira kuwa mfano wa kushiriki katika biashara ya kaboni na kuachana na kasumba kuwa ni ya wageni pekee.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi

slot gacor