Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu Rasmi ya Ofisi ya Makamu wa Rais

Timu ya Soka ya Ofisi ya Makamu wa Rais yaifunga Wizara ya Ardhi 1-0
Jul 24, 2026
Timu ya Soka ya Ofisi ya Makamu wa Rais yaifunga Wizara ya Ardhi 1-0
Timu ya Soka ya Ofisi ya Makamu wa Rais ikishiriki mchezo wa kirafiki na Timu ya Soka ya Wizara ya Ardhi katika mchezo kwenye Uwanja wa Kilimani, jijini Dodoma leo Julai 24, 2026 ambapo iliibuka na ushindi wa goli 1-0.
Na Robert Hokororo

================================================================================================================

Timu ya Soka ya Ofisi ya Makamu wa Rais imeendelea kujinoa kuelekea michuano ya SHIMIWI kwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Timu ya Soka ya Wizara ya Ardhi katika mchezo wa kirafiki uliochezwa kwenye Uwanja wa Kilimani, jijini Dodoma.

Mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa ulizikutanisha timu hizo mbili katika maandalizi ya kuelekea Michuano ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI), inayotarajiwa kufanyika baadaye mwaka huu.

Kwa dakika zote 90, timu zote zilionyesha kiwango kizuri cha ushindani huku zikitengeneza nafasi mbalimbali za kufunga. Hata hivyo, Timu ya Ofisi ya Makamu wa Rais ilifanikiwa kutumia vyema moja ya nafasi zake na kufunga bao pekee la ushindi, lililodumu hadi mwisho wa mchezo.

Michuano ya SHIMIWI hukutanisha watumishi wa Serikali kutoka wizara, idara na taasisi mbalimbali nchini, ikiwa na lengo la kuimarisha afya, mshikamano, ushirikiano na kuibua vipaji vya michezo miongoni mwa watumishi wa umma.

Ushindi huo wa bao 1-0 unaipa Timu ya Soka ya Ofisi ya Makamu wa Rais morali na kujiamini zaidi wakati ikiendelea na programu ya maandalizi kuelekea michuano hiyo muhimu inayotarajiwa kushirikisha timu mbalimbali kutoka taasisi za Serikali nchini.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi

slot gacor