Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu Rasmi ya Ofisi ya Makamu wa Rais

Watumishi Ofisi ya Makamu wa Rais washiriki Mei mazoezi
Jul 04, 2026
Watumishi Ofisi ya Makamu wa Rais washiriki Mei mazoezi
Watumishi wa Ofisi ya Makamu wa Rais leo, Julai 4, 2026, wakishiriki mazoezi ya pamoja yaliyofanyika katika Uwanja wa Shule ya Sekondari Dodoma.
Na Robert Hokororo

Watumishi wa Ofisi ya Makamu wa Rais leo, Julai 4, 2026, wakishiriki mazoezi ya pamoja yaliyofanyika katika Uwanja wa Shule ya Sekondari Dodoma.

=====================================================================================================================
Watumishi wa Ofisi ya Makamu wa Rais leo, Julai 4, 2026, wameshiriki mazoezi ya pamoja yaliyofanyika katika Uwanja wa Shule ya Sekondari Dodoma, ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha utamaduni wa kufanya mazoezi kwa ajili ya kuimarisha afya ya mwili na akili, kuongeza mshikamano miongoni mwa watumishi, pamoja na kujenga ari ya utendaji kazi wenye tija.

Mazoezi hayo yamekuwa sehemu ya jitihada za kuhimiza mtindo bora wa maisha unaochangia ustawi wa watumishi na kuongeza ufanisi katika kutekeleza majukumu ya kila siku ya kuwahudumia wananchi. Ushiriki wa watumishi katika shughuli za michezo na mazoezi pia unaimarisha ushirikiano, nidhamu, umoja na kujenga mazingira bora ya kazi yanayochochea ubunifu na uwajibikaji.

Ofisi ya Makamu wa Rais inaendelea kuhamasisha watumishi wake kushiriki kikamilifu katika shughuli za michezo na mazoezi ya viungo, kwa kutambua kuwa afya njema ni nguzo muhimu ya utumishi wa umma wenye weledi, ufanisi na matokeo chanya kwa maendeleo ya Taifa.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi

slot gacor