
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni akizungumza na wanafunzi pamoja na wananchi mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika ujenzi wa Shule ya Forest ambayo ni mchepuo wa Kiingereza katika Kata ya Kongwe Wilaya ya Kibaha mkoani Pwani wakati akiwa mkoani humo kwa ajili ya ziara ya kikazi, Julai 20,2026.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni (kulia) akimsikiliza Meneja wa mradi katika Kituo cha kupoza umeme Mlandizi wilaya ya Kibaha mkoani Pwani, Mhandisi Josephat Marandu alipofanya ziara katika kituo hicho ambapo yupo mkoani humo kwa ajili ya ziara ya kikazi aliyoianza kuifanya kuanzia, Julai 20,2026.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni (kulia) akimsikiliza Meneja wa mradi katika Kituo cha kupoza umeme Mlandizi wilaya ya Kibaha mkoani Pwani, Mhandisi Josephat Marandu alipofanya ziara katika kituo hicho ambapo yupo mkoani humo kwa ajili ya ziara ya kikazi aliyoianza kuifanya kuanzia, Julai 20,2026.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni (katikati) akimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Nickson John, wakati akiwa Mkoani Pwani kwa ajili ya ziara ya kikazi, Julai 20,2026.
========================================================================================================================
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni amewataka wawekezaji katika sekta ya viwanda kuzingatia uwekezaji unaofuata taratibu na sheria ya Mazingira.
Masauni amesema hayuko tayari kufanya ziara kwa ajili ya kufunga Viwanda vilivyokiuka sheria za Mazingira ambavyo vingekuwa kimbilio kwa vijana na kupunguza tatizo la ajira.
Masauni ameyasema hayo Julai 20, 2026 alipofanya ziara ya kikazi Mkoani Pwani katika Wilaya ya Kibaha na kutembelea miradi mbalimbali ya kimaendeleo ikiwemo kuweka jiwe la Msingi kwenye kituo cha biashara kilichojengwa na Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha na kuweka jiwe la msingi katika ujenzi wa Shule mpya ya mchepuo wa Kiingereza katika Kata ya Kongwe.
"Tunahitaji uwekezaji huu kwa ajili ya watoto wetu hatupendi uwekezaji usiofuata sheria ya mazingira, tuendelee kuhakikisha tunawasiliana na mamlaka za mazingira uwekezaji huu usiwe kero kwa wananchi," amesema
Mhe. Masauni amesema ni muhimu kila mmoja atimize wajibu wake anapofanya uwekezaji katika maeneo mbalimbali hapa nchini iwe faida kwa jamii.
Vijana hawapaswi kuwa watazamaji kwenye uwekezaji uliofanyika Kibaha, ili Wawekezaji walipe kodi watahitaji vijana wanaofanya kazi ndio maana Serikali ikaamua kujenga vituo hivyo kuwaandaa vijana waweze kujiajiri na kuajiriwa.
Amesema Mkoa wa Pwani umekuwa kiungo cha mkoa wa kibiashara wa Dar es Salam na hivyo uwepo wa karakana hiyo ya kisasa karibu na barabarani kuu itahudumia magari yanayotumia njia hiyo.