
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Richard Muyungi akifanya mazungumzo na Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Bw. Ernest Sungura ambaye alimtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo Mei 14, 2026.

Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Bw. Ernest Sungura akieleza jambo wakati wa kikao na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Richard Muyungi ofisini kwa Katibu Mkuu jijini Dar es Salaam leo Mei 14, 2026.

Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Bw. Ernest Sungura akieleza jambo wakati wa kikao na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Richard Muyungi ofisini kwa Katibu Mkuu jijini Dar es Salaam leo Mei 14, 2026.

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Richard Muyungi akikabidhiwa vitabu kuhusu masuala ya habari kutoka kwa Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Bw. Ernest Sungura ambaye alimtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo Mei 14, 2026.

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Richard Muyungi (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Bw. Ernest Sungura mara baada ya kufanya mazungumzi alipomtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo Mei 14, 2026.
==============================================================================================================
Waandishi wa vyombo vya habari nchini wamehimizwa kuwa mstari wa mbele kutangaza mafanikio ya Tanzania kimataifa kupitia utekelezaji wa programu na miradi ya hifadhi ya mazingira nchini.
Hayo yamesemwa Mei 14, 2026 Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Richard Muyungi wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Bw. Ernest Sungura.
Dkt. Muyungi amesema hivi karibuni Tanzania imepata sifa kubwa katika Jumuiya ya Kimataifa katika kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia, ajenda ambayo inapaswa kupaswa sauti na vyombo vya habari nchini.
“Akiwa Dubai katika mkutano wa COP 28, Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan aliongoza mkutano wa pembezoni na kuzindua Programu ya Nishati Safi ya Kupikia kwa Wanawake Barani Afrika…Hili ni jambo kubwa ambalo linalopaswa kupewa msukumo na vyombo vya habari” amesema Dkt. Muyungi.
Akieleza kuhusu uzoefu wake katika tasnia ya habari kimataifa, Dkt. Muyungi amesema waandishi wa habari wamekuwa mstari wa mstari wa mbele kutangaza mafanikio ya mataifa yao hatua inayoharakisha kasi ya maendeleo.
Aidha Dkt. Muyungi amesema uandishi wa habari wa mazingira hauna budi kupewa msukumo na msisitizo wa kipekee katika vyombo vya habari nchini ili kusaidia maendeleo ya jamii na taifa kwa ujumla.
Amesema Ofisi yake ipo tayari kushirikiana na Baraza hilo na wadau wa sekta ya habari nchini kwani ni tasnia muhimu inayosadia wananchi kuweza kupata taarifa za masuala muhimu kuhusu miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali.
Dkt. Muyungi amesema akiwa Mwenyekiti wa Kundi la Majadiliano la Afrika kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (AGN) aliwezesha ushiriki wa waandishi wa vyombo vya habari katika mikutano ya kimataifa ya mazingira hatua iliyolenga kupawa uzoefu na kuwajengea uwezo.
Kwa upande wake, Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Bw. Ernest Sungura amesema Baraza hilo linaendelea kushirikiana na Serikali katika kukuza na kuhimiza weledi katika taaluma ya uandishi wa habari nchini.
“Tumepanga tuwe na tuzo ya waandishi wa habari wabobezi katika mazingira na hili tumewekea msisitizo kwa kuwaandaa wanahabari ambao wanakuwa na uelewa wa masuala ya mazingira” amesema Sungura.