Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu Rasmi ya Ofisi ya Makamu wa Rais

Matukio mbalimbali katika hafla ya uapisho wa viongozi Ofisi ya Makamu wa Rais
Jul 27, 2026
Matukio mbalimbali katika hafla ya uapisho wa viongozi Ofisi ya Makamu wa Rais
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, Waziri Mkuu Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka katika picha ya pamoja na Viongozi mbalimbali kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) mara baada ya uapisho wa Viongozi uliyofanyika Ikulu ndogo, Tunguu Zanzibar, leo tarehe 27 Julai 2026.
Na Robert Hokororo

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Naibu Katibu Mkuu (Muungano) Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Latifa Mohammed Khamis mara baada ya uapisho wa Viongozi uliyofanyika Ikulu ndogo, Tunguu Zanzibar, tarehe 27 Julai 2026.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni, pamoja na Naibu Waziri wa Ofisi hiyo, Mhe. Reuben Kwagilwa, wameshiriki katika hafla ya kuapishwa kwa Naibu Katibu Mkuu (Muungano), Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Latifa Mohamed Khamis, na Naibu Katibu Mkuu (Mazingira), Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Maduhu Isaac Kazi, iliyofanyika leo, Julai 27, 2026, Ikulu Zanzibar.

Viongozi hao waliapishwa mara baada ya kuteuliwa na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kushika nyadhifa hizo.

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Richard Muyungi akiwa na Naibu Katibu Mkuu (Mazingira)  Dkt. Maduhu Kazi wakiwa katika hafla ya uapisho  leo, Julai 27, 2026, Ikulu Zanzibar.

Viongozi hao waliapishwa mara baada ya kuteuliwa na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kushika nyadhifa hizo

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi

slot gacor