
Naibu Katibu Mkuu (Mazingira), Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Maduhu Isaac Kaziakizungumza wakati wa ziara yake ya kikazi katika Wizara hiyo, leo Julai 28, 2026. Mazungumzo hayo yalijikita katika kuimarisha ushirikiano wa kitaasisi katika usimamizi na uhifadhi wa mazingira, biashara ya kaboni na utekelezaji wa ajenda ya uchumi wa buluu.




Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Maduhu Isaac Kazi (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Ofisi ya Makamu wa Rais na Mamlaka ya Usimamizi wa Mazingira Zanzibar (ZEMA), mara baada ya kukamilisha ziara yake ya kikazi katika ofisi za Mamlaka hiyo, leo Julai 28, 2026. Ziara hiyo ilikuwa sehemu ya kuimarisha ushirikiano wa kitaasisi katika usimamizi, uhifadhi wa mazingira na uratibu wa ajenda za biashara ya kaboni na uchumi wa buluu kati ya Tanzania Bara na Zanzibar.