Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akisalimiana na Viongozi mbalimbali wakati alipowasili katika Ukumbi wa Ngurdoto Mkoani Arusha kufungua Mkutano Mkuu wa 13 wa Kitaaluma wa Waandishi Waendesha Ofisi Tanzania (TAPSEA) leo tarehe 21 Mei 2026.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akisalimiana na Mwenyekiti wa Waandishi Waendesha Ofisi Tanzania (TAPSEA) Bi. Zuhura Maganga wakati alipowasili katika Ukumbi wa Ngurdoto Mkoani Arusha kufungua Mkutano Mkuu wa 13 wa Kitaaluma wa Waandishi Waendesha Ofisi Tanzania (TAPSEA) leo tarehe 21 Mei 2026.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akiwa na Viongozi mbalimbali wakishiriki Mkutano wa 13 wa Kitaaluma wa Waandishi wa Waendesha Ofisi Tanzania (TAPSEA) unaofanyika katika Ukumbi wa Ngurdoto Mkoani Arusha. Tarehe 21 Mei 2026.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akipokea tuzo iliyotolewa na Chama cha Waandishi wa Waendesha Ofisi Tanzania (TAPSEA) kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati wa Mkutano Mkuu wa 13 wa Kitaaluma wa Chama hicho unaofanyika katika Ukumbi wa Ngurdoto Mkoani Arusha tarehe 21 Mei 2026. Anayekabidhi ni Mwenyekiti wa Waandishi Waendesha Ofisi Tanzania (TAPSEA) Bi. Zuhura Maganga

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akihutubia wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 13 wa Kitaaluma wa Waandishi wa Waendesha Ofisi Tanzania (TAPSEA) unaofanyika katika Ukumbi wa Ngurdoto Mkoani Arusha. Tarehe 21 Mei 2026.

Waandishi wa Waendesha Ofisi Tanzania wakiimba wimbo pamoja na Kwaya ya Utumishi wa Umma wakati wa Mkutano Mkuu wa 13 wa Kitaaluma wa Chama hicho unaofanyika katika Ukumbi wa Ngurdoto Mkoani Arusha. Tarehe 21 Mei 2026.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanachama wa Chama cha Waandishi wa Waendesha Ofisi Tanzania (TAPSEA) mara baada ya kufungua Mkutano Mkuu wa 13 wa Kitaaluma wa Chama hicho unaofanyika katika Ukumbi wa Ngurdoto Mkoani Arusha. Tarehe 21 Mei 2026.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akiondoka katika Ukumbi wa Ngurdoto mara baada ya Ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 13 wa Kitaaluma wa Waandishi wa Waendesha Ofisi Tanzania (TAPSEA). Tarehe 21 Mei 2026.
===============================================================================================================
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amesema Serikali inatambua umuhimu mkubwa wa Waandishi Waendesha Ofisi kwa kuwa ni muhimili muhimu katika kuwawezesha Viongozi na watendaji kutekeleza majukumu yao.
Makamu wa Rais amesema hayo, wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 13 wa Kitaaluma wa Waandishi wa Waendesha Ofisi Tanzania (TAPSEA) unaofanyika katika Ukumbi wa Ngurdoto Mkoani Arusha. Amesema Serikali inaipa uzito Taasisi ya TAPSEA kwa kuwa inatambua ili kuwa na utulivu na mshikamano ni lazima Waandishi Waendesha ofisi kutimiza wajibu ipasavyo.
Amewapongeza Waandishi Waendesha Ofisi kwa kubeba sura za Taasisi wanazofanyia kazi kwa kuwa wakarimu na wenye kutoa msaada wa awali kwa wananchi wanaofika kutafuta huduma. Amewasihi kuendelea kutoa huduma kwa ukamilifu pamoja na kuwa na heshima na ukarimu ili kuwafariji wanaowahudumia.
Aidha Makamu wa Rais, amewasisitiza waandishi waendesha ofisi kuendelea kujitambua na kutunza siri wakati wa utekelezaji wa majukumu yao.
Makamu wa Rais amekipongeza Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania kwa kuimarisha elimu yao mpaka kufikia shahada ya uzamili ambayo imewawezesha Waandishi Waendesha Ofisi kuhama katika mfumo asili wa utekelezaji wa majukumu yao mpaka kufikia kuwa sehemu ya maamuzi ya kisera na upangaji wa mikakati na utekelezaji wake.
Amesisitiza kwamba Vyuo vinavyotoa mafunzo hayo, vinapaswa kuendelea kujiimarisha ili kuwa na waandishi waendesha ofisi wanaoweza kusaidia vema Taifa. Makamu wa Rais ametoa wito kwa Taasisi mbalimbali kuhakikisha wanawawezesha Waandishi Waendesha Ofisi kushiriki mikutano ya kitaaluma.
Halikadhalika, Makamu wa Rais amewapongeza Viongozi wa Taasisi hiyo wanaomaliza muda wao kwa kufanya kazi nzuri iliyowaunganisha na kuwawezesha Waandishi Waendesha Ofisi nchini. Aidha amewataka kufanya uchaguzi wa haki ili kupata Viongozi sahihi wanataoiongoza vema Taasisi hiyo. Amewasihi kufanya uchaguzi kwa kuzingatia uhuru na haki ili kupata viongozi sahihi wa Taasisi hiyo pamoja na kuwataka wanachama kuchagua viongozi makini bila ubaguzi wa aina yeyote.
Kwa upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete, amesema Serikali kupitia ofisi hiyo, itaendelea kutoa ushirikiano kwa watumishi wote wa Umma ikiwemo uongozi wa TAPSEA ili kufanikisha masuala mbalimbali ya kiutumishi kwa wanachama wake.
Ameongeza kwamba, Ofisi hiyo itaendelea kuwaangalia na kuwalea wanaTAPSEA na kuwataka kuwa na imani na serikali inayoongozwa na Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwa wataendelea kuwaangalia katika hali zote kiwemo maslahi yao, kutoa mafunzo pamoja na kuwahakikisha kuwa salama muda wote.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Waandishi Waendesha Ofisi Tanzania (TAPSEA) Bi. Zuhura Maganga amesema Taasisi hiyo inajivunia mafanikio yaliyopatikana katika kuimarisha taaluma ya uandishi uendesha ofisi ikiwemo kuanzishwa kwa shahada ya utawala inayotolewa na Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania pamoja kuanzishwa kwa shahada ya uzamili ya Sanaa katika mawasiliano na usimamizi wa ofisi.