Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu Rasmi ya Ofisi ya Makamu wa Rais

Masauni ashiriki hafla ya Maadhimisho ya Katiba ya Norway
May 16, 2026
Masauni ashiriki hafla ya Maadhimisho ya Katiba ya Norway
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais ( Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamadi Yussuf Masauni akishiriki katika hafla ya Maadhimisho ya Siku ya Katiba ya Norway, iliyofanyika Dar es Salaam, Mei 15, 2026. Mhandisi Masauni ameelezea kuwa urafiki huo wa takribani Miaka 60 umesaidia kujenga ushirikiano katika nyanja mbalimbali ikiwa ni pamoja na miradi inayosaidia katika Uhifadhi na utunzaji wa Mazingira.
Na Robert Hokororo

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais ( Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamadi Yussuf Masauni akishiriki hafla ya Maadhimisho ya Siku ya Katiba ya Norway, iliyofanyika Dar es Salaam, Mei 15, 2026. Mhandisi Masauni ameelezea  kuwa urafiki huo wa takribani Miaka 60 umesaidia kujenga ushirikiano katika nyanja mbalimbali ikiwa ni pamoja na miradi inayosaidia katika Uhifadhi na utunzaji wa Mazingira.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais ( Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamadi Yussuf Masauni akishiriki hafla ya Maadhimisho ya Siku ya Katiba ya Norway, iliyofanyika Dar es Salaam, Mei 15, 2026. Mhandisi Masauni ameelezea  kuwa urafiki huo wa takribani Miaka 60 umesaidia kujenga ushirikiano katika nyanja mbalimbali ikiwa ni pamoja na miradi inayosaidia katika Uhifadhi na utunzaji wa Mazingira.

================================================================================================================

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. Mhandisi Hamadi Yussuf Masauni amesema katika miaka ya hivi karibuni, biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Norway imeongezeka kwani hadi kufikia Desemba 2025, Mamlaka ya Uwekezaji ilisajili jumla ya miradi 46 ya uwekezaji kutoka Norway, yenye makadirio ya thamani ya dola za Kimarekani milioni 323.062, na kuongeza zaidi ya ajira 4,400.

Amesema ushirikiano kati ya Tanzania na Norway una zaidi ya miongo sita ambapo nchi hizi zikiwa zimejenga urafiki wenye mizizi katika uaminifu, kuimarishwa kwa mshikamano, na kuhamasishwa na kushirikiana.

Mhe. Masauni amesema urafiki wa Tanzania na Norway ambao umevumilia mabadiliko katika siasa za kimataifa na mabadiliko katika uchumi wa kimataifa.

“Tunathamini ushirikiano unaoendelea wa Norway na Tanzania katika maeneo kama vile kustahimili hali ya hewa, nishati mbadala, kilimo endelevu, elimu, na utawala bora.

Waziri Masauni ameyasema hayo wakati wa hafla ya ya Maadhimisho ya Siku ya Katiba ya Norway iliyofanyika Dar es Salaam, Mei 15, 2026 akieleza kuwa urafiki huo umesaidia kujenga zaidi ya miradi inayosaidia katika uhifadhi na utunzaji wa mazingira.

“Tunaipongeza Norway kwa uongozi wake imara hasa katika nyanja za kimataifa namna unavyoendelea kustawi hasa ukijikita katika kusaidia suala zima la uhifadhi na utunzaji wa mazingira eneo ambalo Ofisi ya Makamu wa Rais ndio yenye dhamana ya kulisimamia hapa nchini,”

“Tanzania inaithamini Norway sio tu kama mshirika wa maendeleo bali pia kama rafiki anayeaminika. Na urafiki, kama daraja, ni nguvu zaidi inapojengwa kutoka pande zote mbili.” Amesema Mhe. Masauni.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi

slot gacor