Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu Rasmi ya Ofisi ya Makamu wa Rais

Serikali yasisitiza umuhimu wa kulinda bahari
May 20, 2026
Serikali yasisitiza umuhimu wa kulinda bahari
Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais, Balozi Baraka Luvanda (kulia) akifungua kikao kazi cha maandalizi ya Kongamano la 11 la Bahari Yetu “11th OUR OCEAN CONFERENCE”. Kilichofanyika leo Zanzibar, Mei 20,2026.
Na Robert Hokororo

Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais, Balozi Baraka Luvanda (kulia) akifungua kikao kazi cha maandalizi ya Kongamano la 11 la Bahari Yetu “11th OUR OCEAN CONFERENCE”. Kilichofanyika leo Zanzibar, Mei 20,2026.

Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais, Balozi Baraka Luvanda akiwa katika picha ya pamoja na viongozi na washiriki baada ya kufungua kikao kazi cha maandalizi ya Kongamano la 11 la Bahari Yetu “11th OUR OCEAN CONFERENCE”. Kilichofanyika leo Zanzibar, Mei 20,2026.

==============================================================================================================

Serikali ya Tanzania imeendelea kusisitiza umuhimu wa kulinda Bahari na rasilimali za majini ili kuhakikisha mazingira ya Bahari yanabaki salama na yenye manufaa kwa kizazi cha sasa na kijacho. 

Ameyazungumza hayo Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais, Balozi Baraka Luvanda wakati akifungua kikao kazi cha maandalizi ya Kongamano la 11 la Bahari Yetu “11th OUR OCEAN CONFERENCE”. Kilichofanyika leo Zanzibar, Mei 20,2026.

“Maneno haya matatu -Bahari Yetu, Urithi Wetu, Mustakabali Wetu kutoka kwenye kauli mbiu ya Kongamano yanabeba uzito mkubwa wa falsafa na wajibu, yanakumbusha kwamba bahari si tu chanzo cha Samaki na madini ila ni sehemu ya utambulisho wetu, historia yetu na tegemeo la vizazi vijavyo” aliendelelea kusisitiza.

Pamoja na hayo Balozi Baraka Luvanda ameweka rai kwamba lengo la kikao hicho ni kufanya maandalizi ya kina ya ushiriki kama nchi, na kuandaa nyaraka zote muhimu kwa ajili ya viongozi kushiriki katika matukio mbali mbali yaliyoandaliwa pamoja na kusisitiza ushirikiano ili kuhakikisha malengo tarajiwa kama nchi wakati wa ushiriki katika Kongamano hilo yanafikiwa.

Tanzania imepokea mwaliko wa heshima kutoka Serikali ya Jamhuri ya Kenya kwa ajili ya kushiriki katika Kongamano la 11 la Bahari yetu (11th Our Ocean Conference) linalo tarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 16-18 Juni 2026, ambapo hii ni mara ya kwanza Kongamano hili kufanyika katika nchi za Afrika.

Lengo la Kongamano hili ni moja ya jitihada za Kimataifa katika kutunza, kuhifadhi na kutumia bahari kwa uendelevu na ustahimilivu wa mabadiliko ya Tabianchi katika Bahari, Uvuvi endelevu ,Uchumi wa Buluu endelevu, maeneo lindwa ya bahari, pamoja na Usalama wa baharini.

Kutokana na umuhimu wa Kongamano hili Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amemteua Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi kumuwakilisha katika Kongamano hilo jijini Mombasa nchini Kenya.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi

slot gacor