Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu Rasmi ya Ofisi ya Makamu wa Rais

Tanzania kuhakikisha upatikanaji wa fedha za mabadiliko ya tabianchi
May 22, 2026
Kaimu Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Martha Ngalowera, kwa niaba ya Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Richard Muyungi akisoma hotuba ya ufunguzi wa Kikao cha Wataalamu cha Maandalizi ya Mkutano wa 64 wa Wataalamu wa Mabadiliko ya Tabianchi (Pre-SB64) wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi, jijini Dodoma leo Mei 22, 2026.
Na Robert Hokororo

Kaimu Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Martha Ngalowera, kwa niaba ya Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Richard Muyungi akisoma hotuba ya ufunguzi wa Kikao cha Wataalamu cha Maandalizi ya Mkutano wa 64 wa Wataalamu wa Mabadiliko ya Tabianchi (Pre-SB64) wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi, jijini Dodoma leo Mei 22, 2026.

Mratibu wa Mikutano ya COP Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Evansia Shirima akitoa maneno ya awali wakati wa Kikao cha Wataalamu cha Maandalizi ya Mkutano wa 64 wa Wataalamu wa Mabadiliko ya Tabianchi (Pre-SB64) wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi, jijini Dodoma leo Mei 22, 2026.

Mratibu wa Mikutano ya COP Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Evansia Shirima akitoa maneno ya awali wakati wa Kikao cha Wataalamu cha Maandalizi ya Mkutano wa 64 wa Wataalamu wa Mabadiliko ya Tabianchi (Pre-SB64) wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi, jijini Dodoma leo Mei 22, 2026.

Mratibu wa Mradi wa TIF wa Shirika la ActionAid Bi. Happay Sanga akizungumza wakati wa Kikao cha Wataalamu cha Maandalizi ya Mkutano wa 64 wa Wataalamu wa Mabadiliko ya Tabianchi (Pre-SB64) wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi, jijini Dodoma leo Mei 22, 2026.

Washriki mbalimbali wakiwa katika Kikao cha Wataalamu cha Maandalizi ya Mkutano wa 64 wa Wataalamu wa Mabadiliko ya Tabianchi (Pre-SB64) wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi, jijini Dodoma leo Mei 22, 2026.

Washriki mbalimbali wakiwa katika Kikao cha Wataalamu cha Maandalizi ya Mkutano wa 64 wa Wataalamu wa Mabadiliko ya Tabianchi (Pre-SB64) wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi, jijini Dodoma leo Mei 22, 2026.

========================================================================================

Tanzania imeweka kipaumbele cha kuhakikisha upatikanaji wa fedha za mabadiliko ya tabianchi ikiwemo utekelezaji wa utoaji wa Dola za Marekani bilioni 300 kwa mwaka na utekelezaji wa Mpango ujulikanao kama Baku to Belem Roadmap wa kuwezesha upatikanaji wa Dola za Marekani trilioni 1.3 kila mwaka ifikapo mwaka 2035. 

 

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Richard Muyungi katika hotuba ya ufunguzi wa Kikao cha Wataalamu cha Maandalizi ya Mkutano wa 64 wa Wataalamu wa Mabadiliko ya Tabianchi (Pre-SB64) wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi, jijini Dodoma leo Mei 22, 2026.

 

Katika hotuba hiyo, iliyosomwa kwa niaba yake na Kaimu Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Martha Ngalowera Dkt. Muyungi alitaja vipaumbele vingine kuwa ni Kutekeleza Kikamilifu Malengo ya Dunia ya Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi (GGA) kwa kuweka viashiria mahususi ili kuweza kufuatilia maendeleo na kuongeza ufadhili wa kukabiliana na madhara ya tabianchi.

 

Aidha, alisema katika mkutano huo unaotarajiwa kufanyika jijini Bonn, Ujerumani kuanzia Juni 08 hadi 18, 2026, Tanzania itahimiza ulinzi wa maeneo ya pwani, bahari na maziwa makuu dhidi ya athari za mabadiliko ya tabianchi kama vichocheo vikuu vya uchumi wa buluu ambao Ofisi ya Makamu wa Rais inaratibu.

 

Halikadhalika, Dkt. Muyungi alitaja kipaumbele kingine kuwa ni Kufuatilia masuala muhimu kuhusu uanzishwaji wa Mfuko wa Kuhifadhi Misitu ya Kitropiki ili kutoa Kipaumbele kwa Maliasili na Misitu kwakutunza misitu, kuhifadhi bionuwai na kuchochea maendeleo endelevu na namna nchi itanufaika na fursa ya fedha za utekelezaji wa miradi ya hifadhi ya misitu.

 

“Matarajio ya nchi katika mkutano huo ni Kuongeza kiwango cha fedha kwenye mfuko wa Upotevu na Hasara yaani Loss & Damage Fund ili kuwezesha utekelezaji wenye ufanisi wa Mfuko huo katika kukabliana na hasara na uharibifu unaochangiwa na mabadiliko ya tabianchi,” alisisitiza.

 

Hivyo, Dkt. Muyungi alisema ushiriki wa Tanzania katika mkutano wa Wataalamu wa Mabadiliko ya Tabianchi (SB64) unaonesha utayari wa pamoja wa kuimarisha hatua za kupambana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

 

Alisema mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabianchi si jukumu la Serikali pekee bali ni la wote ikiwa ni pamoja na wadau wa maendeleo, sekta binafsi, mashirika yasiyokuwa ya kiserikali, sekta binafsi, wanawake, vijana, watoto, makundi maalum na jamii nzima wanashirikishwa na kuelewa vipaumbele vya nchi vilivyoainishwa kuelekea SB64 ili kuwa na msimamo jumuishi wa kitaifa. 

 

Akitoa maneno ya awali, Mratibu wa Mikutano ya COP Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Evansia Shirima alisema malengo mahususi ya mkutano huo wa wataalamu ni kupitia na kuanisha vipaumbele vya kitaifa na misimamo ya majadiliano ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika maeneo muhimu ya SB64, ikiwemo kuandaa Msimamo wa Nchi utakaoeleza vipaumbele hivyo, ujumbe muhimu na matokeo yanayotarajiwa.

Alisema pia, kikao kitakuza ushirikishwaji wa wadau mbalimbali kwa kuhakikisha sauti za watoto, vijana, wanawake, kundi la watu wenye ulemavu, Asasi za kiraia na wadau wote muhimu zinajumuishwa kikamilifu katika mchakato wa uandaaji wa msimamo wa nchi.

Bi. Evansia aliongeza kuwa wataalamu katika kikao wamepata nafasi ya kupanga namna bora ya ushiriki wa nchi katika mkutano wa SBs kwa kutumia jukwaa husika kuonesha dunia hatua za mbalimbali ambazo nchi inazichukua katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Naye Mratibu wa Mradi wa TIF kutoka Shirika la ActionAid Bi. Happay Sanga alishukuru Ofisi ya Makamu wa Rais kwa uratibu mzuri wa mikutano ya kimataifa ambayo inatoa fursa kwa wadau na makundi mbalimbali kushiriki.

Alisema majadiliano ya watalaamu jatika mkutano huo yanaweza kuleta tija na suluhisho la changamoto ya mabadiliko ya tabianchi ikiwemo ukame, mafuriko yanaathiri jamii.

 

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi

slot gacor