Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Bi. Mary Maganga (wa pili kushoto) akifuatilia semina kuhusu magonjwa yasiyoambukiza iliyokuwa ikitolewa na Madaktari pamoja na wataalamu mbalimbali kutoka Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH), Machi 22, 2024 kwa watumishi wa Ofisi ya Makamu wa Rais.

Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu Ofisi ya Makamu wa Rais, Bw. Elisha Msengi akifuatilia semina ya magonjwa yasiyoambukiza iliyokuwa ikitolewa kwa Watumishi wa Ofisi ya Makamu wa Rais na madaktari pamoja na wataalamu mbalimbali kutoka Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) jijini Dodoma Machi 22,2024.

Kaimu Mkurugenzi idara ya Mazingara Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Kemilembe Mutasa akifuatilia semina kuhusu magonjwa yasiyoambukiza kwa watumishi wa Ofisi ya Makamu wa Rais iliyotolewa na Madaktari pamoja na wataalamu mbalimbali kutoka Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH), Machi 22, 2024.

Mkurugenzi wa Mafunzo na Utafiti Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) Monica Kessy akizungumza wakati wa Mafunzo ya magonjwa yasiyoambukiza kwa watumishi wa Ofisi ya Makamu wa Rais.

Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais Bi, Christina Mndeme (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na madaktari na wataalamu mbalimbali kutoka Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) baada ya kufunga semina ya magonjwa yasiyoambukiza iliyokuwa ikitolewa kwa wafanyakazi wa ofisi hiyo jijini Dodoma leo Machi 22,2024. Kulia kwake, Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu Ofisi ya Makamu wa Rais, Bw. Elisha Msengi.

Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais Bi, Christina Mndeme (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali baada ya kufunga semina ya magonjwa yasiyoambukiza iliyotolewa na madaktari pamoja na wataalamu mbalimbali kutoka Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) kwa wafanyakazi wa ofisi hiyo jijini Dodoma leo Machi 22,2024. Kulia kwake (waliokaa) Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu Ofisi ya Makamu wa Rais, Bw. Elisha Msengi na kushoto kwake ni Dk. Jesse Jonathan mtaalamu wa magonjwa ya saratani kutoka Hospitali ya Benjamin Mkapa. Waliosimama wa kwanza kushoto Mkurugenzi wa Kitengo cha Menejimenti ya Ununuzi Bi. Juliana Mkalimoto, Kaimu Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Rasilimaliwatu Bw. Obeid Ndahoze na Mkuu wa Kitendo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Sarah Kibonde.

=============================================================================

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Bi. Mary Maganga amesema ni vyema kuwa wazi juu ya kulinda afya zetu sababu itasaidia kupata msaada wa kusaidiwa haraka na kupatiwa matibabu.

Ameyasema hayo wakati wa semina kuhusu magonjwa yasiyoambukiza kwa watumishi wa Ofisi ya Makamu wa Rais iliyotolewa na Madaktari pamoja na wataalamu mbalimbali kutoka Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) jijini Dodoma Machi 22, 2024.

Bi. Maganga amesema afya njema kwa binadamu ni mtaji katika maisha yake sababu hakuna anayeweza kufanya vyema majukumu yake kama afya yake haiko imara hivyo kila mmoja anatakiwa kuijua afya yake.

“Naamini semina hii itazaa matunda kwetu baada ya kupata elimu juu ya magonjwa mbalimbali katika kulinda afya zetu,” anasema Bi. Maganga.

Naye, Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais Bi, Christina Mndeme ameongeza kuwa, kutokana na umuhimu wa elimu iliyotolewa na wataalamu hao ipo haja ya kupanga siku nyingine ili kuweza kusaidia wafanyakazi wa Ofisi ya Makamu wa Rais kupewa zaidi elimu juu ya afya.

“Naamini hakuna aliyetoka kama alivyoingia, tumejifunza mambo mengi sahivi tumejua chakula kipi kinapaswa kuliwa kwa wakati upi hayo yote baada ya mtaalamu wa Lishe na Chakula kutufundisha lakini tumeweza kujifunza dalili za magongwa mbalimbali na namna ya kujikinga,” amesema Bi. Mndeme.

Hata hivyo, Mkurugenzi wa Mafunzo na Utafiti Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) Bi. Monica Kessy amesema wafanyakazi wanatakiwa kuwa na utaratibu wa kupima afya zao kila wakati jambo ambalo litawasaida kujua hali ya afya zao.

Aidha, mtaalamu wa chakula na Lishe kutoka Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH), Yasinta Luambano amesema ili kulinda afya ni vyema kupunguza matumizi ya vyakula vilivyoongezwa sukari kama vile soda na juisi za viwandani zilizoongezwa ladha ya matunda.

“Punguzeni ulaji wa vyakula vilivyokaangwa na mafuta mengi, mafuta yenye lehemu nyingi, mafuta yaliyotengenezwa viwandani yenye lehemu nyingi au sukari au chumvi pia nashauri mtu kula matunda badala ya kunywa juisi sababu unapokula matunda inakuwa vyema zaidi kiafya.”

Ameongeza kuwa ni muhimu kuzingatia ulaji unaofaa ilikuzuia na kupunguza magonjwa sugu yasiyo ya kuambukiza.

Katika semina hiyo watumishi walifundishwa mambo mbalimbali kama vile kuhusu Ugonjwa wa Saratani, figo, kisukari, Shinikizo la damu, Afya ya Akili pamoja na Lishe.

By admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *