Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dkt.Selemeni Jafo akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi mitungi ya gesi 1500 yakiwa na majiko yake kwa wananchi wa Jiji la Arusha wakiwemo wajasiriamali tarehe 27 Aprili,2024 jijini Arusha Mikutano Arusha  

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dkt.Selemeni Jafo na viongozi mbalimbali wakikabidhi mitungi ya gesi ya kupikia wa Oryx kwa mama lishe wa Mkoa wa Arusha wakati wa hafla ya kukabidhi mitungi ya gesi 1,500 yakiwa na majiko yake kwa wananchi wa Jiji la Arusha wakiwemo wajasiriamali tarehe 27 Aprili, 2024.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dkt.Selemeni Jafo akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya gesi ya Oryx Bw. Benoite Aramanwakati wa hafla ya kukabidhi mitungi ya gesi 1,500 yakiwa na majiko yake kwa wananchi wa Jiji la Arusha wakiwemo wajasiriamali tarehe 27 Aprili, 2024.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dkt.Selemeni Jafo akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wakati wa hafla ya kukabidhi mitungi ya gesi 1,500 yakiwa na majiko yake kwa wananchi wa Jiji la Arusha wakiwemo wajasiriamali tarehe 27 Aprili, 2024.

===========================================================================

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemeni Jafo amesema takwimu zinaonesha watu milioni nne barani Afrika wanapoteza maisha kila mwaka kutokana na matumzi ya nishati chafu ikiwemo ya kuni na mkaa.

Hivyo, amesema ajenda ya Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuanzisha kampeni ya kuhamasisha nishati safi Afrika inapaswa kuungwa mkono na watu wote.

Amesema kuwa matumizi ya kuni na mkaa nchini yanasababisha hekta takriban 46,242 kupotea kila mwaka kwa kukatwa kwa ajili ya kupata kuni na mkaa.

Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi mitungi ya gesi 1,500 yakiwa na majiko yake kwa wananchi wa Jiji la Arusha tarehe 27 Aprili, 2024 wakiwemo wajasiriamali, Dk. Jafo amesema hatua hiyo inaunga mkono juhudi za Rais Samia katika kampeni ya kuhamasisha nishati safi.

“Rais Dk.Samia Suluhu Hassan amekuwa na dhamira njema na ndio maana amekuja na kampeni ya nishati safi ya kupikia.Haya ni mapenzi yake na kwasababu tunafahamu nishati chafu inamadhara makubwa katika mazingira.

“Kwanza watu wanalazimika kutegemea kuni na mkaa kwa hiyo kuna uharibifu wa mazingira. Takwimu zinaonesha kila mwaka hekta 4,6242 zinapotea kwasababu ya kuni na mkaa,”amesema Dkt. Jafo.

Pia amesema takwimu zinaonesha kuwa wakinamama na wasichana kwa asilimia kubwa wanatumia wastani wa saa 20 kwa wiki kwa ajili ya kutafuta kuni na mkaa au wakati mwingine ni kinyesi cha wanyama.

“Leo hii ukiona nchi imejipanga katika nishati safi ya kupia ni jambo la msingi lenye kutia matumani.Watafiti  wanatuambia kitendo cha kutumia nishati safi ya kupikia kwa akina mama wajazito kunasaidia kurekebisha presha ya mama mjazito,”amesema.

Ameongeza pia nishati safi inasaidia mama mjazito kupata mtoto mwenye uzito unaokubalika anapozaliwa , hivyo kuna faida nyingi  kutumia nishati safi ya kupikia.

“Nina fahamu mpaka leo hii Oryx wameshatoa mitungi ya gesi 32,000 kwa ajili ya jamii na wameshatumia Sh.bilioni 2.7 lakini bado wameendelea kuendelea na kampeni hiyo kwa kutoa mitungi kwa jamii.

Ameongeza kuwa Oryx wamekuwa mfano mzuri kuifikia jamii  huku akifafanua tayari Serikali imeshatoa maelekezo kwa taasisi zinazoanzia watu 100 kufunga mfumo wa kutumia nishati safi ya kupikia na tayari taasisia na mashirika ya umma yameanza kutumia nishati hiyo.

Kwa upande wake Mbunge wa Arusha Mjini Mrisho Gambo amesema katika kuunga mkono jitihada za Rais Dk.Samia kuhamasisha nishati safi ya kupikia wameona ni vema kuendelea kuyagusa makundi mbalimbali katika jimbo hilo.

Amesema kuwa kabla ya kugawa mitungi hiyo 1,500 ya Oryx kwa wana Arusha Mjini, tayari ameshagawa pia mitungi 1400 kwa wajasiriamali huku akisisitiza wataendelea na kuyafikia makundi yote yakiwemo ya watoto wanaolelewa vituo vya ya watoto yatima.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya gesi ya Oryx Bw. Benoite Araman amesema madhara yanayotokana na kutumia kuni na mkaa ani makubwa na kuwa wananchi 33,000 wanapoteza maisha kila mwaka kwa kuvuta moshi na chembe chembe zinazotokana na mkaa na kuni, hivyo kupikia gesi itatatua jambo hili.

Amesema kupika kwa kutumia gesi huchochea kutokukatwa kwa miti kwa ajili ya  kuni na mkaa hivyo, husaidia kulinda mazingira na wakati huo huwafanya wanawake wasitumie muda mwingi kutafuta kuni na msituni hatua itakayosaidia maandalizi ya chakula kwa wakati.

“Oryx Gas Tanzania itaendelea kufanya kazi kwa bidii ili kutekeleza maono ya Rais kuhusu upatikanaji wa nishati. Namshukuru Mbunge wa Arusha Mjini Gambo na Serikali ya Tanzania kwa kutuunga mkono katika mipango yetu ya nishati safi kwa kuhakikisha matumizi ya gesi ya Oryx hapa Arusha na Tanzania kwa ujumla,”. Amesema Bw. Araman

Wakitoa shukrani zao Wajasiriamali Bi. Asha Mtumwa na Bw. Karim Abdallah wakieleza kuwa hatua hiyo ya kukabidhiwa mitungi ya gesi inakwenda kuwaondolea adha waliyokuwa wakiipata kwa muda mrefu.

Wamesisitiza kuwa inaenda kuondoa athari ambazo zimekuwa zikijitokeza kwa matumizi ya kuni na mkaa ambapo inaathari kuanzia kwenye afya pamoja na mazingira sanjari na kuokoa gharama za mkaa ambazo ni kubwa zaidi.

By admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *