Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akizungumza wakati wa hafla fupi ya kuwaaga watendaji wastafu kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) iliyofanyika usiku wa tarehe 27 Aprili, 2024 jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Dkt. Immaculate Semesi wakati wa hafla fupi ya kuwaaga watendaji wastaafu wa baraza hilo iliyofanyika usiku wa tarehe 27 Aprili, 2024 jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akimkabidhi Mkurugenzi Mkuu Mstaafu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Mhandisi Dkt. Samuel Gwamaka wakati wa hafla fupi ya kuwaaga watendaji wastaafu wa baraza hilo iliyofanyika usiku wa tarehe 27 Aprili, 2024 jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo na viongozi mbalimbali wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) wakiwatakia heri na kuwapongeza watendaji wastaafu wa Baraza hilo katika hafla fupi iliyofanyika usiku wa tarehe 27 Aprili, 2024 jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akiwa katika ya pamoja na viongozi mbalimbali wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) katika hafla fupi iliyofanyika usiku wa tarehe 27 Aprili, 2024 jijini Dar es Salaam.

=============================================================================

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo ameshiriki hafla fupi ya kuwaaga watendaji wastafu kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) iliyofanyika usiku wa tarehe 27 Aprili, 2024 jijini Dar es Salaam.

Miongoni mwa wastaafu walioagwa ni Dkt.Samuel Gwamaka aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu NEMC, Bw.Lewis Nzali aliyekuwa Meneja wa Kanda ya Kaskazini na Bw. Anold Kisiraga. Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Waziri Dkt. Jafo amemshukuru Dkt. Gwamaka kwa kuwa msaada mkubwa katika kufanikisha majukumu yake kama Waziri mwenye dhamana ya Mazingira.

Amesema kuwa alipoingia Ofisi ya Makamu wa Rais hakuwa anafahamu mengi kuhusu mazingira lakini kutokana na uwepo wa Dkt. Gwamaka aliweza kutekeleza majukumu yake kwa urahisi.

Akitoa salamu kwa niaba ya Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhandisi Cyprian Luhemeja, Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Bi. Christina Mndeme amewapongeza wastaafu hao na kusifu utendaji kazi wa Dkt. Gwamaka.

“Kwakweli tunaufurahia, tunauenzi, tunauamini na tunauthamini utendaji wako na umeacha alama kwenye Baraza na hata hii mifuko ya plastiki tulijiuliza kama tutaweza lakini tuliweza kwa sababu ulitoka na ukasema.” Amesema Bi. Christina.

Akitoa neno kwenye hafla hiyo Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi NEMC Mhandisi Profesa Esnat Chaggu amesema wakati wanaanza kutekeleza Majukumu yao walikuta malalamiko mengi sana lakini kwa kushirikiana na Dkt. Samuel Gwamaka waliweza kuyapunguza Kwa kiasi kikubwa.

Hafla hiyo ilihudhuriwa pia na viongozi na watendaji kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais na NEMC wakiwemo Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Bi. Christina Mndeme, Mwenyekiti na Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi NEMC Prof. Esnat Chaggu, Mkurugenzi Mkuu NEMC Dkt. Immaculate Semesi na Kaimu Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Kemilembe Mutasa.

Katika hafla hiyo pia, NEMC iliwaaga watumishi wa Idara ya Fedha waliopata fursa ya kulitumikia Taifa nje ya Baraza ambao ni Mhasibu Mkuu Bi. Esther Subi na Mkurugenzi wa Utawala Bw. Charles Wangwe

By admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *