Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis akizungumza na wananchi wa kata ya Ihusi-Bariadi, Mkoani Simiyu katika mkutano wa hadhara wakati kamati ya mawaziri 8 wa kisekta wanaoshughulikia migogoro ya ardhi ya vijiji 975.

Sehemu ya wananchi wa kata ya Ihusi-Bariadi, Mkoani Simiyu wakimsikiliza Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis (hayupo pichani) katika mkutano wa hadhara wakati kamati ya mawaziri 8 wa kisekta wanaoshughulikia migogoro ya ardhi ya vijiji 975.

=================================================================

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis amewataka viongozi wa mikoa na wilaya nchini kwenda kuwafundisha wananchi namna bora ya kusimamia sheria na taratibu za utunzaji na uhifadhi wa vyanzo vya maji.

Pia ametaka viongozi hao kuelimisha namna ya kufuata na kutekeleza sheria zitakazolinda mazingira, ardhi na maliasili wakiwemo wanyamapori na mapori ya akiba.

Mhe. Khamis aametoa kauli hiyo kwa nyakati tofauti wakati akizungumza na uongozi wa Mkoa wa Simiyu pamoja na wananchi wa kata ya Ihusi-Bariadi, Mkoani Simiyu katika mkutano wa hadhara wakati kamati ya mawaziri 8 wa kisekta wanaoshughulikia migogoro ya ardhi ya vijiji 975.

Alisema, miongoni mwa vitu vikubwa ambavyo Kamati ya Mawaziri wa Wizara za Kisekta imebaini wakati wa ziara zake ni upungufu na uchache wa usimamizi wa seheria hasa zile sheria za mazingira.

Kwa mujibu wa Mhe. Khamis moja ya njia sahihi ya kutatua migogoro ya matumizi ya ardhi bila kuleta taharuki kama ilivyoelekezwa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ni kwenda kuwafundisha wananchi kipi kipo kwenye sheria .

“’Twendeni kufundisha namna bora ya kusimamia sheria na taratibu za utunzaji na uhifadhi vyanzo vya maji, ni masafa gani wananchi wanatakiwa kufuga ama kujenga kutoka chanzo cha maji maana kinyume na hapo kila siku tutakuwa tunalia mazingira, maliasili, ardhi plus migogoro’’, alisema.

Naibu Waziri huyo alibainisha kwa kusema kuwa, bila kutoa elimu ya namna ya kusimamia sheria na taratibu za utunzaji na uhifadhi mazingira serikali itaingia mzigo mkubwa wa kuzunguka, kusema na kueleza tu kwa sababu tu kuna mambo hayajasemwa mwanzo.

“Tukawaambie watu wetu watunze vyanzo vya maji kinyume na hapo hatutakuwa na maliasili, hatutakiwa na rasilimali kwa sababu vyanzo vya maji ni fahari yetu watanzania,” alisisitiza.

By admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *