Katibu Mkuu Maganga aongoza Kikao cha Kamati ya Uongozi ya Mradi wa EBARR

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Bi. Mary Maganga akiongoza Kikao cha Kamati ya Uongozi ya Mradi wa Kuhimili Mabadiliko ya tabianchi kwa kutumia Mifumo Ikolojia Vijijini (Ecosystem Based Adaptation for Rural Resilience – EBARR in Tanzania) kilichofanyika jijini Dodoma leo Mei 12, 2021.
Katibiu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Bi. Maganga ambaye pia ni Mwenyekiti Kamati ya Uongozi ya Mradi wa Kuhimili Mabadiliko ya tabianchi kwa kutumia Mifumo Ikolojia Vijijini (Ecosystem Based Adaptation for Rural Resilience – EBARR in Tanzania) aliwaongoza wajumbe wanaounda kamati hiyo kutoka Wizara, wawakilishi kutoka Taasisi za Serikali na asasi zisizo za kiserikali pamoja na Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) kupitia taarifa ya utekelezaji wa mradi huo ya mwaka 2020.
Wajumbe wa Kamati ya Uongozi ya Mradi wa Kuhimili Mabadiliko ya tabianchi kwa kutumia Mifumo Ikolojia Vijijini (Ecosystem Based Adaptation for Rural Resilience – EBARR in Tanzania) wakiwa katika Kikao cha kupitia taarifa ya utekelezaji wa mradi huo ya mwaka 2020. Pia wajumbe hao walipitia bajeti ya mwaka wa 2021 na mpango kazi wa manunuzi wa mwaka 2021.

By admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *