Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo akizungumza wakati akizindua Mpango Mkakati wa Taifa wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi wa mwaka 2021 hadi 2026 pamoja na Kongamano la Mazingira ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani leo Juni 4, 2021 katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Centre jijini Dodoma.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Hamad Hassan Chande akizungumza wakati wa wa uzinduzi wa Mpango Mkakati wa Taifa wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi wa mwaka 2021 hadi 2026 pamoja na Kongamano la Mazingira ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani leo Juni 4, 2021 katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Centre jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Bi. Mary Maganga akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mpango Mkakati wa Taifa wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi wa mwaka 2021 hadi 2026 pamoja na Kongamano la Mazingira ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani leo Juni 4, 2021 katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Centre jijini Dodoma.
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Shirika la CARE International Tanzania, Bi. Haika Mtuiakizungumza wakati akizindua Mpango Mkakati wa Taifa wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi wa mwaka 2021 hadi 2026 pamoja na Kongamano la Mazingira ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani leo Juni 4, 2021 katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Centre jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo akiwa na viongozi na wadau wa maendeleo wakionesha Mpango Mkakati wa Taifa wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi wa mwaka 2021 hadi 2026 baadfa ya kuuzindua ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani.
===========================================================================================

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo amesema kwa mujibu wa wataalamu asilimia moja ya Pato la Taifa linapotea kila mwaka kutokana na mabadiliko ya tabianchi.

Jafo amesema hay oleo Juni 4, 2021 wakati akizindua Mpango Mkakati wa Taifa wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi wa mwaka 2021 hadi 2026 pamoja na Kongamano la Mazingira ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani.

Alisema pamoja na takwimu hizo pia inakadiriwa kuwa zaidi ya watu milioni 1.6 wa ukanda wa pwani watakabiliwa na changamoto za mazingira ifikapo mwaka 2030 ikiwa jamii haitaacha shughuli za kibinadamu zinazoathiri mazingira.

Hivyo kutokana na tishio hilo Waziri Jafo ameitaka jamii kutofanya shughuli zinazohatarisha uhifadhi wa mazingira.

“Kutokana na mapinduzi ya viwanda na shughuli za kibinadamu zimeweza kuchangia mabadiliko ya tabianchi na bila kulinda mazingira, dunia haitokuwa sehemu salama na uchumi wa mataifa mengi utadidimia hivyo kuna haja kwa nchi zilizoendelea kuzisaidia nchi maskini kupambana na athari za zinazosababishwa na mabadiliko ya tabianchi,” alisisitiza.

Aidha, Waziri huyo alisema kuwa miongoni mwa mafanikio yaliyopatikana kupitia Mkakati wa Mabadiliko ya Tabianchi wa mwaka 2012 alisema umewezesha utekelezaji wa miradi mbalimbali ambayo imesaidia katika kuhigfadhi mazingira.

Miongoni mwa miradi hiyo ni ujenzi wa ukuta kando ya Bahari ya Hindi ambao umesaidia kupunguza kasi ya mawimbi ya bahari pamoja na mradi wa mabasi yaendayo haraka (DART) ambao unasaidia kupunguza hewa ya ukaa.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Shirika la CARE International Tanzania, Bi. Haika Mtui aliipongeza Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kuwa na ushirikiano katika kuhamasisha jamii kuhusu utunzaji wa mazingira.

By admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *