Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Maganga akizungumza na watumishi wa Ofisi yake katika kikao kazi cha kujadili masuala ya kiutendaji na uwajibikaji kilichofanyika leo Julai 19, 2021 jijini Dodoma. 
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu, Bw. Mbuli Shelusi akitoa neno la ukaribisho kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Maganga kuzungumza na watumishi katika kikao kazi cha kujadili masuala ya kiutendaji na uwajibikaji kilichofanyika leo Julai 19, 2021 jijini Dodoma. 
Watumishi wa Ofisi ya Makamu wa Rais wakiwa katika kikao na Katibu Mkuu Bi. Mary Maganga cha kujadili masuala ya kiutendaji na uwajibikaji kilichofanyika leo Julai 19, 2021 jijini Dodoma. 
Watumishi Ofisi ya Makamu wa Rais wakiwa wamesimama kwa dakika moja kumkumbuka aliyekuwa mtumishi mwenzao Marehemu George Kafumu aliyefariki hivi karibuni kabla ya kuanza kwa kikao kazi na Katibu Mkuu Bi. Mary Maganga leo Julai 19, 2021 jijini Dodoma. 

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Maganga hii leo amekutana na watumishi wa Ofisi yake katika kikao kazi cha kujadili masuala ya kiutendaji na uwajibikaji katika kutekeleza majukumu ya  Ofisi ya Makamu wa Rais. Pia, Bi. Mary Maganga ametoa rai kwa watumishi hao kuendelea kufanya kazi kwa weledi, uadilifu na uzalendo kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na taratibu katika mwaka mpya wa fedha. Aidha, ametumia nafasi hiyo kuwaasa watumishi kuwa utaratibu wa kufanya tathmini ya utendaji kazi wao wa kila siku na kuweka malengo.Sambamba na masuala ya kiutendaji, Bi. Mary Maganga pia ametumia fursa hiyo kuwashauri watumishi kuhusu masuala mbalimbali ya kijamii ambayo kwa namna moja au nyingine yana mchango mkubwa katika ufanishi wa utendaji kazi wa watumishi mahala pa kazi. Masuala hayo ni pamoja na afya na lishe, kujenga tabia ya kufanya mazoezi, kushiriki shughuli za kijamii na kuendelea kuzingatia maelekezo ya Wizara ya Afya kujikinga na janga la UVIKO 19.

ReplyForward

By admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *