Muonekano wa Banda moja lenye vyumba vinne vya kusomea wanafunzi wa skuli ya Msingi Kangagani likiwa limeshamalizika na linatumika, lililojengwa na wafadhili mbali mbali kupitia mbunge wa jimbo la Kojani Kisiwani Pemba.
Wanafunzi na wajumbe wa kamati ya skuli na kamati ya ujenzi wa banda moja la skuli lenye vyumba vinne vya kusomea, wakifuatilia kwa makini hafla ya makabidhiano ya jengo hilo, kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la Kojani ambaye ni Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Hamad Hassan Chande,kwenda kwa kamati ya skuli ya msingi Kangani.
Mbunge wa Jimbo la Kojani Kisiwani Pemba na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Hamad Hassan Chande, akiandika ubaoni katika moja ya darasa la wanafunzi ikiwa ni ishara ya kukabidhi banda moja lenye vyumba vinne vya kusomea wanafunzi kwa uongozi wa kamati ya skuli ya msingi Kangagani Wilaya ya Wete.
Mbunge wa Jimbo la Kojani Kisiwani Pemba na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Hamad Hassan Chande, akikagua mitihani ya majaribio ya wanafunzi wa Kidato cha nne skuli ya msingi Kangagani.
Mbunge wa Jimbo la Kojani Kisiwani Pemba na Naibu waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Hamad Hassan Chande (katikati), akiitikia dua maalumu iliyoombwa kwa ajili yake na wajumbe wa kamati ya skuli ya Msingi Kangagani, baada ya kuwakabidhi banda la kisasa lenye vyumba vinne vya kusomea wanafunzi.

By admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *