Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo akitoa maelekezo ya Serikali kwa Bw. Is-haka Juma msimamizi wa mgodi wa Double F kuhusu takwa la kisheria la kufanya ukaguzi wa mazingira katika eneo la uchenjuaji wa dhahabu. Wa pili kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Rorya Bw. Juma Chikoka na Mbunge wa Jimbo la Rorya Mhe. Jafari Chege.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo akitoa maelekezo ya Serikali kwa Bw. Is-haka Juma msimamizi wa mgodi wa Double F kuhusu takwa la kisheria la kufanya ukaguzi wa mazingira katika eneo la uchenjuaji wa dhahabu. Wa pili kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Rorya Bw. Juma Chikoka na Mbunge wa Jimbo la Rorya Mhe. Jafari Chege.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Selemani Jafo amesitisha shughuli za uchenjuaji wa dhahabu katika mtambo wa double F katika kijiji cha Nyakisya Wilayani Tarime kutokana na uchafuzi wa mazingira.

Agizo hilo amelitoa hii leo Mkoani Mara kufuatilia malalamiko ya wananchi kuhusu athari za kiafya na kimazingira zinazo sadikika zinazotokana na kemikali ya cyanide inayotumika katika shughuli za uchenjuaji wa dhahabu na kutiririka katika chanzo cha maji cha Senye.

Akizungumza kwa niaba ya wakazi wa maeneo hayo, Mwenyekiti wa Mtaa wa Nyakihenene Bw. Mwita Ngusui amesema kuwa wakazi wengi na vitongoji vya maeneo ya jirani kwa kiasi kikubwa wameathirika na kemikali ya cyanide

Kufuatia hatua hiyo Jafo amesema kikosi kazi kinachoundwa na Taasisi za Serikali ikiwa ni pamoja na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Mamlaka ya Mkemia Mkuu na Bodi ya Bonde la Ziwa Victoria kwa pamoja kuchunguza na kutoa taarifa za kitaalamu kuhusu maji hayo ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa.

Jafo amesema Ofisi yake haitamvumilia mwekezaji yeyote anaeharibu mazingira na kuathiri afya za watu.

Katika hatua nyingine Waziri Jafo amebaini  ukikwaji wa Sheria ya Mazingira ya mwaka 2004 kwa mgodi huo wa double F kwa kuanza shughuli ya uchenjuaji bila kufanya Tathmini ya Athari kwa mazingira.

Amemwelekeza Msimamizi wa Mtambo huo wa double F Bw. Is-haka Juma kuwalisiliana na Ofisi za Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) mapema iwezekanavyo ili ukaguzi wa mazingira uweze kufanyika.

Akizungumza kwa niaba ya wakazi wa maeneo hayo Mwenyekiti wa Mtaa wa Nyakihenene Bw Mwita Ngusui amesema kuwa wakazi wengine wa maeneo hayo na vitongoji vya jirani kwa kiasi kikibwa wameathirika na kemikali hiyo.

Nae Mbunge wa Jimbo la Rorya Mhe. Jafari Chege ameishukuru Serikali kwa kusikia kilio cha wananchi wa Rorya kwa kufanya ufuatiliaji wa haraka.

By admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *