Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya pamoja ya Serikali ya Muungano ya Tanzania (SMT) na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) wanaoshughulikia masuala ya Muungano wakisikiliza maelezo kuhusu kiwanda cha Azam na Mji wa Fumba kutoka kwa Mtendaji katika Kiwanda hicho (hakupatikan jina) wakati wa  Ziara ya Wajumbe wa Kamati ya pamoja ya Serikali ya Muungano ya Tanzania (SMT) na Serikali ya Mapimduzi ya Zanzibar (SMZ) wanaoshughulikia masuala ya Muungano iliyoanzia kiwandani hapo nakumalizikia Uwanja wa Ndege wa Abeid Amani Karume jengo la abiria TERMINAL 3.
Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi , Mhe. Rahma Kassim ali akijibu hoja zinazohusiana na jengo la abiria TERMINAL 3 wakati wa  Ziara ya Wajumbe wa Kamati ya pamoja ya Serikali ya Muungano ya Tanzania (SMT) na Serikali ya Mapimduzi ya Zanzibar (SMZ) wanaoshughulikia masuala ya Muungano iliyoanzia kiwanda kinachozalisha maziwa   cha Azam Fumba nakumalizikia katika Uwanja wa Ndege wa Abeid Amani Karume Zanzibar.
Wazri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira ) Mhe. Selemani Jafo akitaka ufafanuzi zaidi juu ya changamoto za kiwanda cha kuzalisha maziwa cha Azam kutoka kwa Mkuu wa Viwango vya Bidhaa katika kiwanda hicho Tumaini Fredrik, wakati wa  Ziara ya Wajumbe wa Kamati ya pamoja ya Serikali ya Muungano ya Tanzania (SMT) na Serikali ya Mapimduzi ya Zanzibar (SMZ) wanaoshughulikia masuala ya Muungano iliyoanzia kiwandani hapo nakumalizikia Uwanja wa Ndege  wa Abeid Amani.
Wajumbe wa Kamati ya pamoja ya Serikali ya Muungano ya Tanzania (SMT) na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) wanaoshughulikia masuala ya Muungano wakisikiliza maelezo kuhusu kiwanda cha Azam na Mji wa Fumba kutoka kwa Mtendaji katika Kiwanda hicho (hakupatikan jina) wakati wa  Ziara ya Wajumbe wa Kamati ya pamoja ya Serikali ya Muungano ya Tanzania (SMT) na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) wanaoshughulikia masuala ya Muungano iliyoanzia kiwandani hapo nakumalizikia Uwanja wa Ndege wa Abeid Amani Karume jengo la abiria TERMINAL 3.

========================================================================

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Selemani Jafo amesema hoja mbalimbali za Muungano zinaendelea kushughulikiwa na Kamati ya Pamoja ili kuhakikisha zinapatiwa ufumbuzi wa kudumu.

Akizungumza mara baada ya ziara ya wajumbe wa Kamati hiyo  walipotembelea kiwanda cha Maziwa Fumba na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume katika jengo la (Terminal III).

 Amesema miradi hiyo ya kimkakati ni miongoni mwa hoja za Muungano ambazo zinatafutiwa ufumbuzi na kamati ya pamoja ili kuhakikisha ufumbuzi unapatikana kwa lengo la kuimarisha  umoja uliopo.

Aliwataka wananchi wafahamu kuwa serikali zote mbili bado zinaendelea kukaa pamoja na kujadili hoja mbalimbali za muungano kwa maslahi ya wananchi.

Nae waziri wa Fedha na Mipango wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mwigulu Nchemba amesema tayari hoja mbalimbali katika masuala ya fedha zimepatiwa fumbuzi ikiwemo suala la fedha  kutoka  uhamiaji  na kodi ya ongezeko la thamani.

 Alieleza kuwa ulipaji wa kodi upande mmoja unamuwezesha mwananchi kupata unafuu na kurahisisha mzunguko wa biashara nchini.

Alisema juhudi zinazoendelea kuchukuliwa na Serikali ya Zanzibar katika kuimarisha Viwaja vya Ndege ni muhimu kwa maendeleo kwani majengo ya kisasa yanasaidia katika kuimarisha sekta ya utalii nchini.

Aliwataka wanachi kuendelea kushirikiana na viongozi wao katika kutunza miundombinu ili waweze kuimarisha zaidi viwanja vya ndege kwa lengo la kukuza uchumi wa nchi.

By admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *