Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Selemani Jafo akitoa maelekezo kwa walimu wa Shule ya Msingi Muhimbili na Umoja wa Mataifa baada ya kuwasili katika viwanja vya shule ya Muhimbili  na  Umoja wa Mataifa Jijijini Dar es Salaam.
Uongozi wa Jumuiya ya Ismaili wakiwa katika picha ya Pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Selemani Jafo.

====================================================================

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Selemani Jafo, ametoa wito kww kila mwananchi ashiriki katika kulinda na kuhifadhi mazingira  kwa mustakabali wa nchi yetu ili iendelee kubaki salama.
Ameyasema hayo alipokuwa Mgeni Rasmi kweye hadhara ya maadhimisho ya Jumuiya ya Ismaili iliyofanyika Jijini Dar es salaam katika Shule ya Msingi Muhimbili na Umoja wa Mataifa. 
Mhe. Jafo alifurahishwa na Jumuiya hiyo kwa kuangazia upande wa mazingira ambapo alisema ameona ni jambo jema la kuhamasisha na kusisitiza jamii kusimamia na kulinda mazingira.
“Tumeona mmefanya kwa vitendo Zaidi katika suala la utunzaji wa mazingira na tumeshiriki kwa pamoja katika upandaji miti ambalo ni jambo zuri na inapendeza, itakuwa mfano katika jiji letu la Dar es Salaam na kwa Tanzania nzima,” alisema.
Aliongeza kuwa suala la upandaji miti na kuweka elimu ya mazingira kwa watoto na uzalendo ni vitu vilimvyomfurahisha na kuwa endapo Jumuiya mbalimbali za dini zitaiga mfano mzuri wa Ismaili, Tanzania itakuwa salama kwa upande wa mazingira.
“Tuendelee kupanda miti na tupunguze matumizi ya mkaa na kuni kwani hali ya kimazingira kwa sasa inatisha sisi Watanzania kwa umoja wetu tuungane kwa pamoja kuepusha athari ya mabadiliko ya Tabianchi. Taifa limeingia katika uchumi wa Kati ili tuweze kwenda mbele Zaidi basi tunahaja ya kulinda na kuhifadhi mazingira yetu.” Amesema Mhe. Jafo 
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mhe. Ng’wilabuzu Ludigija amesema kuwa Jumuiya hii imeonyesha mfano kwa jumuiya zingine kwani wanashiriki katika masuala mbalimbali ya kijamii ikiwemo  usafi na utunzaji wa mazingira pia katika maafa mbalimbali Jumuiya hiyo imekuwa mstari wa mbele. 
Naye Mwakilishi wa Taasisi ya Aga Khan Nchini Tanzania Amin Kurji ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa kujenga Mazingira wezeshi kwa wawekezaji binafsi katika maendeleo ya jamii ya Tanzania, na jinsi hali hiyo ilivyo muhimu kwa kazi  za kuleta mendeleo. Urafiki kati ya Ismaili Imamat na Taasisi zake na Serikali ya Tanzania ni wa muda mrefu na wa manufaa.

By admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *