Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway anayeshughulikia Maendeleo ya Kimataifa na Nchi za NORDIC Mhe. Anne Veathe Tvinnereim akipokelewa na mwenyeji wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo alipowasili Ofisi hizo jijini Dodoma kwa ajili ya kufanya mazungumzo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akifanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway anayeshughulikia Maendeleo ya Kimataifa na Nchi za NORDIC Mhe. Anne Veathe Tvinnereim pamoja na ujumbe wake katika ukumbi wa Ofisi ya Makamu wa Rais jijini Dodoma.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway anayeshughulikia Maendeleo ya Kimataifa na Nchi za NORDIC Mhe. Anne Veathe Tvinnereim akimkabidhi zawadi mwenyeji wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo mara baada ya kufanyika kwa kikao katika ukumbi wa Ofisi ya Makamu wa Rais jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akikabidhi kitabu cha Mpango Kabambe wa Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (2022-2032) kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway anayeshughulikia Maendeleo ya Kimataifa na Nchi za NORDIC Mhe. Anne Veathe Tvinnereim mara baada ya kufanyika kwa kikao katika ukumbi wa Ofisi ya Makamu wa Rais jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway anayeshughulikia Maendeleo ya Kimataifa na Nchi za NORDIC Mhe. Anne Veathe Tvinnereim (wa pili kushoto), Balozi wa Norway nchini Tanzania Mhe. Elisabeth Jacobsen (kushoto) na Balozi wa Tanzania nchini Norway Mhe.Grace Olotu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe kutoka Serikali ya Norway na viongozi na wataalamu kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais mara baada ya kumalizika kwa kikao.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akiagana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway anayeshughulikia Maendeleo ya Kimataifa na Nchi za NORDIC Mhe. Anne Veathe Tvinnereim na Balozi wa Norway nchini Tanzania Mhe. Elisabeth Jacobsen baada ya kikao katika Ofisi ya Makamu wa Rais jijini Dodoma.

===================================================================

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway anayeshughulikia Maendeleo ya Kimataifa na Nchi za NORDIC Mhe. Anne Veathe Tvinnereim leo Septemba 8, 2022 jijini Dodoma.

Katika mazungumzo hayo Waziri Jafo alishukuru Norway kwa ushirikiano wake kwa Tanzania hatua iliyochangia maendeleo katika sekta za afya, elimu na miundombinu na kusema ushirikiano huo uliodumu kwa takriban miaka 55 uendelee.

Alisema uhifadhi wa mazingira unaoonekana ni kutokana na juhudi zinazofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye amekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha nchi inakuwa salama katika sekta ya mazingira.

Dkt. Jafo alisema Serikali ya Tanzania inatarajia kushirikiana na Serikali ya Norway katika usimamizi na matumizi endelevu ya rasilimali zinazopatikana baharini bila kuathiri hifadhi ya mazingira.

Alisema upo mpango kazi wa kuhakikisha mazingira ya bahari yanakuwa salama dhidi ya changamoto ya taka za plastiki ambazo ni hatari kwa maisha ya viumbe wa baharini.

Waziri Jafo alisema eneo lingine kuwa ni kuiwezesha kamati ya kitaifa ya uchumi wa bluu kufanya kazi zake kwa ufanisi sambamba na kuhakikisha upandaji wa mikoko unakuwa endelevu ili kusaidia kupunguza athari za mabadiliko ya tabianchi.

Kwa upande wake Waziri Tvinnereim amepongeza juhudi za Serikali ya Tanzania kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais katika kupambana na changamoto za uharibifu wa mazingira.

Amesema kuwa Tanzania imepiga hatua kubwa katika mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabianchi kwani imeweza kuandaa Sera ambazo zinachochea katika kulinda na kuhifadhi mazingira.

Pia waziri huyo aliahidi kuwa Serikali ya Norway iko tayari kuongeza nguvu katika jitihada zinazofanyika hapa nchini ili kufikia malengo ya kuwa na Tanzania inapata matokeo mazuri katika uhifadhi wa mazingira.

Naye Balozi wa Norway nchini Mhe. Elisabeth Jacobsen alisifu Tanzania kwa jitihada za kupambana na athari za mabadiliko ya tabianchi ambazo zimekuwa zikihatarisha usalama wa chakula.    

Kikao hicho kilihudhuriwa na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Dkt. Switbert Mkama, Balozi wa Tanzania nchini Norway Mhe.Grace Olotu pamoja na wataalamu kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais.

By admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *