Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Dkt. Switbert Mkama akifungua Warsha ya Kukuza uelewa wa Wataalamu kuhusu Sera ya Taifa ya Mazingira na Usimamizi wa Matumizi Salama ya Bioteknolojia ya kisasa kwa niaba ya Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Maganga, leo Oktoba 27, 2022 jijini Dodoma.
Washiriki wakiwa katika Warsha ya Kukuza uelewa wa Wataalamu kuhusu Sera ya Taifa ya Mazingira na Usimamizi wa Matumizi Salama ya Bioteknolojia ya kisasa iliyofanyika leo Oktoba 27, 2022 jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Chama cha Bioteknolojia nchini Prof. Peter Msolla, akitoa neno kabla ya hotuba ya ufunguzi wa Warsha ya Kukuza uelewa wa Wataalamu kuhusu Sera ya Taifa ya Mazingira na Usimamizi wa Matumizi Salama ya Bioteknolojia ya kisasa leo Oktoba 27, 2022 jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Andrew Komba neno la utangulizi kabla ya ufunguzi wa Warsha ya Kukuza uelewa wa Wataalamu kuhusu Sera ya Taifa ya Mazingira na Usimamizi wa Matumizi Salama ya Bioteknolojia ya kisasa leo Oktoba 27, 2022 jijini Dodoma.
Afisa Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Onesphory Kamukuru akiwasilisha mada kuhusu Sera ya Taifa ya Mazingira (2021) wakati wa Warsha ya Kukuza uelewa wa Wataalamu kuhusu Sera ya Taifa ya Mazingira na Usimamizi wa Matumizi Salama ya Bioteknolojia ya kisasa leo Oktoba 27, 2022 jijini Dodoma.
Mhadhiri na Mtafiti kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Dkt. Ally Mahadhy akiwasilisha mada kuhusu Bioteknolojia ya kisasa, Matumizi yake, Faida na Changamoto zilizopo wakati wa warsha hiyo.
Afisa Mazingira Mwandamizi kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Thoams Chali akiwasilisha mada kuhusu Usimamizi wa Matumizi Salama ya Bioteknolojia ya kisasa nchini, Matumizi yake, Faida na Changamoto zilizopo wakati wa warsha hiyo.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Dkt. Switbert Mkama akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Warsha ya Kukuza uelewa wa Wataalamu kuhusu Sera ya Taifa ya Mazingira na Usimamizi wa Matumizi Salama ya Bioteknolojia ya kisasa leo Oktoba 27, 2022 jijini Dodoma.

===================================================================

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Dkt. Switbert Mkama,amewataka wataalamu kutoka wizara za kisekta kutekeleza Sera ya Taifa ya Mazingira ya mwaka 2021 ili kuwa na usimamizi thabiti wa matumizi salama ya bioteknolojia ya kisasa kwa maendeleo endelevu ya taifa. 

Hayo ameyasema  leo Oktoba 27,2022 jijini Dodoma na wakati akifungua Warsha ya kukuza uelewa kwa wataalam hao kuhusu usimamizi wa matumizi salama ya Bioteknolojia ya kisasa kwa niaba ya Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Maganga,

Dkt. Mkama amesema ni muhimu kujenga uwezo wa taasisi na kukuza uelewa wa jamii kuhusu teknoljia hii ili kuhakikisha tunafaidika na teknolojia hii katika sekta husika na kupunguza uwezekano wa kutokea kwa athari zozote za afya ya binadamu na mazingira.

Ameeleza kuwa wataalamu hao wana jukumu la kutoa ushauri stahiki kuhusu masuala haya ili Serikali kwa kuzingatia vipaumbele na maslahi ya nchi inapofikia maamuzi ya matumizi ya teknolojia hii katika sekta yoyote nchini.

“Katika kuhakikisha kunakuwa na usalama wa matumizi ya bioteknolojia ya kisasa nchini, Serikali imeandaa na kuweka nyenzo mbalimbali za usimamizi wa teknolojia hii ikiwa ni pamoja na Sheria ya Usimamizi wa Mazingira ya mwaka 2004, Mfumo wa Kitaifa wa Usimamizi wa Matumizi Salama ya Bioteknolojia ya Kisasa 2007, Kanuni za Matumizi Salama ya Bioteknolojia ya Kisasa ya mwaka 2009 na marekebisho yake ya mwaka 2015 na Miongozo mbalimbali za mwaka 2010,” amesema .

Aidha, amefafanua kuwa Tanzania ni nchi mwanachama wa Mkataba wa Kimataifa ya Hifadhi ya Bioanuai ambao una malengo makuu matatu yakiwemo Hifadhi ya bioanuai; Matumizi endelevu ya bioanuai na Mgawanyo sahihi wa faida zitokanazo na matumizi ya bioanuai. 

Ameongeza kuwa Tanzania iliridhia Mkataba huu Machi 1996, ili kuweza kushirikiana na Jumuiya ya Kimataifa katika kutekeleza malengo hayo.

Pia, amesema ibara ya 19 ya Mkataba huu, inaainisha, umuhimu wa nchi wanachama kuweka mazingira wezeshi ya kutumia biotekinolojia ya kisasa kwa maendeleo endelevu. 

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Bioteknolojia nchini Prof. Peter Msolla, amesema warsha hiyo ni muhimu kwani inakutanisha wataalamu mbalimbali kuweza kubadilishana mawazo ili mwisho wa siku kupata maamuzi yenye tija.

Prof.Msolla amesema kuwa bioteknolojia sio mpya ni tasnia ya zamani ambayo imekuwa ikibadilika kadiri ya wakati na haina tofauti sana na uzalishaji wa mazao kwa njia ya kiasili lakini tofauti yake kubwa ni muda wa matokeo.

Naye Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Andrew Komba amesema tunahitaji mijadala mingi zaidi kuhusu usimamizi wa matumizi salama ya bioteknolojia ya kisasa ili kuweza kufanya maamuzi sahihi.

By admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *