Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akifunua kitambaa kama ishara ya kuzindua josho la kuogeshea mifugo katika Kijiji cha Irkujit wilayani Simanjiro mkoani Manyara ambalo limejengwa kupitia Mradi wa Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi kwa kutumia Mifumo Ikolojia Vijijini (EBARR).

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akiangalia mifugo ambayo inasubiri kuogeshwa katika josho ambalo amezindua katika Kijiji cha Irkujit wilayani Simanjiro mkoani Manyara ambalo limejengwa kupitia Mradi wa Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi kwa kutumia Mifumo Ikolojia Vijijini (EBARR).
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akiangalia kiatu alitembelea kikundi cha mradi wa uchakataji na utengenezaji wa bidhaa za ngozi Kijiji cha Jitegemee wilayani Simanjiro mkoani Manyara ambao unatekelezwa kupitia Mradi wa Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi kwa kutumia Mifumo Ikolojia Vijijini (EBARR).
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akiwa katika ziara ya kukagua Mradi wa Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi kwa kutumia Mifumo Ikolojia Vijijini (EBARR) wilayani Simanjiro mkoani Manyara.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Irkujit wilayani Simanjiro mkoani Manyara alipofanya ziara ya kukagua Mradi wa Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi kwa kutumia Mifumo Ikolojia Vijijini (EBARR).
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akivishwa vazi maalumu la Kimasai alipofanya ziara ya kukagua Mradi wa Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi kwa kutumia Mifumo Ikolojia Vijijini (EBARR).
Mkuu wilaya ya Simanjiro Dkt. Suleiman Serera akitoa neno kwa wananchi wa Kijiji cha Irkujit wilayani Simanjiro mkoani Manyara wakati wa ziara Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo alipofanya ziara ya kukagua Mradi wa Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi kwa kutumia Mifumo Ikolojia Vijijini (EBARR).
Mbunge wa Jimbo la Simanjiro Mhe. Christopher Ole Sendeka akitoa neno kwa wananchi wa Kijiji cha Irkujit wilayani Simanjiro mkoani Manyara wakati wa ziara Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo alipofanya ziara ya kukagua Mradi wa Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi kwa kutumia Mifumo Ikolojia Vijijini (EBARR).

==================================================================

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo amezindua josho la kuogeshea mifugo katika Kijiji cha Irkujit wilayani Simanjiro mkoani Manyara ambalo limejengwa kupitia Mradi wa Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi kwa kutumia Mifumo Ikolojia Vijijini (EBARR).

Akizungumza na wananchi wakati wa ziara ya kukagua mradi huo Desemba 15, 2022 amewapongeza wananchi hao kwa kuibua mradi huo ambao unawawezesha kuikinga mifugo yao kwa magonjwa yaenezwayo na kupe na mbung’o.

Dkt. Jafo amesema josho hilo linalotarajiwa kuhudumia wananchi takriban 30,000 wa kijiji hicho na vijiji jirani ni matunda ya Serikali katika kuhakikisha inawasidia wananchi kupambana na athari za mabadiliko ya Tabianchi.  

Alisema athari za mabadiliko ya tabianchi ni kubwa zinazosababisha maeneo ya nchi kuwa na ukame ambao ni chanzo cha kukosekana kwa mvua, hivyo matokeo yake ni kukauka kwa vyanzo vya maji vikiwemo mabwawa.

“Ndugu zangu leo hii ukienda Mto Ruaha ambao ndio chanzo cha maji kinachopeleka katika Bwawa la Mtera umekauka, pia Kidatu maji yamepungua na ndio maana tumeshuhudia baadhi ya maeneo yanapata mgao wa umeme, hayo yote ni mabadiiko ya tabianchi,” amesema Dkt. Jafo.

Aliweka bayana kuwa ili kukabiliana na changamoto kama hizo, Ofisi ya Makamu wa Rais inatekeleza Mradi wa EBARR katika baadhi ya vijiji ambavyo vinakabiliwa na changamoto ya ukame ili kuwasaidia wananchi wa maeneo hayo.

Waziri huyo ameupongeza uongozi wa wilaya hiyo kwa kuisimamia mradi hiyo katika eneo lao huku akitoa rai kwa wananchi wa Wilaya ya Simanjiro kuitunza ili isiharibiwe na idumu kwa ajili ya vizazi vijavyo.

Katika ziara hiyo pia alitembelea na kukagua miradi mingine ikiwemo wa kikundi cha uzalishaji wa bidhaa za ngozi na ujenzi wa bwawa linalotarajiwa kusaidia upatikanaji wa maji ambao unaendelea kutekelezwa kupitia EBARR.

Hata hivyo ameonesha kutoridhishwa na mwenendo wa utekelezaji wake ambao ameelekeza watalaamu ngazi ya wilaya wanaousimamia wahakikishe unarekebishwa dosari zote zilizojitokeza na kukamilika kwa wakati ili kuendana na thamani ya fedha iliyotengwa kwa ajili ya ujenzi huo.

Kutokana na kuchelewa kukamilika kwa mradi huo Waziri Jafo amemuelekeza mkandarasi aliyepewa kazi hiyo kuukamilisha ifikapo Januari 15, 2023 ili uanze kuhudumia maelfu ya wananchi wa kijiji hicho ikiwa ni hatua ya Serikali ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Dk. Suleiman Serera ameishukuru Ofisi ya Makamu wa Rais kwa ujumla kwa kupelekea mradi huo wilayani humo ambako kuna changamoto ya ukame.

Amesema ni dhahiri kuwa kazi inaonekana kupitia katika shughuli mbalimbali zinazofanywa na wanavikundi vikiwemo ufugaji wa nyuki ambao wanatumia misitu iliyofadhiwa.

Aidha, Dkt. Serera ameiomba Ofisi ya Makamu wa Rais kupanua wigo wa mradi huo katika maeneo mengine kwa kuwa wafugaji wengi wanahitaji majosho ya kuogeshea mifugo ili kukabiliana na athari za maabdiliko ya tabianchi.

Wakizungumza kwa niaba ya wananchi Mbunge wa Jimbo la Simanjiro Mhe. Christopher Ole Sendeka na Diwani wa Kata ya Irujit pia wamepongeza juhudi za Serikali katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi wilayani humo.

Viongozi hao wawili pia watumia nafasi hiyo kutoa wito kwa Ofisi ya Makamu wa Rais kuongeza vijiji katika utekelezaji wa mradi huo ili wananchi wengi zaidi wafaidike nao.   

Katika ziara ya hiyo Waziri Dkt. Jafo amepewa heshima ya Laigwanani na Jamii ya Wamasai kutoka Wilaya ya Simanjiro.

Mradi wa EBARR unatekelezwa pia katika wilaya za Mpwapwa (Dodoma), Mvomero (Morogoro), Kishapu (Shinyanga) na Kaskazini ‘A’ iliyopo Mkoa wa Kaskazini (Zanzibar).

By admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *