Viongozi mbalimbali kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais pamoja na Wakufunzi wa mafunzo elekezi (induction) wakiwa kwenye picha ya pamoja na watumishi wapya kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais baada ya kumaliza mafunzo hayo yaliyokuwa yakiendeshwa na Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) mkoani Morogoro kuanzia Oktoba 16 hadi 19, 2023.

Kaimu Mkurugenzi Idara ya Rasilimali Watu Ofisi ya Makamu wa Rais, Bw. Elisha Msengi akifunga mafunzo elekezi (induction) leo Oktoba 19, 2023 yaliyokuwa yakitolewa kwa watumishi wapya wa Ofisi ya Makamu wa Rais. Mafunzo hayo yanatolewa kwa lengo la kujifunza Sheria, Kanuni na taratibu za utumishi wa Umma na zile zinazotumika katika uendeshaji wa Serikali. Mafunzo hayo yameendeshwa na Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) mkoani Morogoro kuanzia Oktoba 16, 2023.

Kaimu Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Usimamizi wa Rasilimali Watu Ofisi ya Makamu wa Rais, Bw. Obeid Ndahoze akisisitiza jambo katika mafunzo elekezi (induction) yaliyokuwa yakitolewa kwa watumishi wapya wa Ofisi ya Makamu wa Rais. Mafunzo hayo yameendeshwa na Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) mkoani Morogoro kuanzia Oktoba 16 hadi 19, 2023.

Bw. John Nzunda Mkufunzi kutoka Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) tawi la Mtwara, akitoa mafunzo elekezi kwa watumishi wapya Ofisi ya Makamu wa Rais yaliyofanyika mkoani Morogoro kuanzia Oktoba 16, 2023.

: Bw. Oswin Clement Mkufunzi kutoka Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) tawi la Mtwara, akitoa mafunzo elekezi kwa watumishi wapya Ofisi ya Makamu wa Rais yaliyofanyika mkoani Morogoro kuanzia Oktoba 16, 2023.

Bw. Gasper Kisinza Mkufunzi kutoka Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) Dar es Salaam, akitoa mafunzo elekezi kwa watumishi wapya Ofisi ya Makamu wa Rais yaliyofanyika mkoani Morogoro kuanzia Oktoba 16, 2023.

Viongozi mbalimbali kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais pamoja na Wakufunzi wa mafunzo elekezi (induction) wakiwa kwenye picha ya pamoja na watumishi wapya kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais baada ya kumaliza mafunzo hayo yaliyokuwa yakiendeshwa na Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) mkoani Morogoro kuanzia Oktoba 16 hadi 19, 2023.

By admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *