Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Maganga akizungumza wakati wa hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na Shirika la Maendeleo la Ujerumani (GIZ) Novemba 16, 2023 jijini Dodoma na kuhudhuriwa na Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Mhe. Thomas Terstegen pamoja na viongozi mbalimbali kutoka Tanzania Bara na Zanzibar.

Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Mhe. Thomas Terstegen akizungumza wakati wa hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na Shirika la Maendeleo la Ujerumani (GIZ) Novemba 16, 2023 jijini Dodoma ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Maganga.

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Maganga akisikiliza maelezo kuhusu shughuli zinazofanywa na Shirika la Maendeleo la Ujerumani (GIZ) wakati wa hafla ya chakula cha jioni jijini Dodoma leo Novemba 16, 2023. Wa pili kulia ni Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Mhe. Thomas Terstegen.

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Maganga akisalimiana na Kamishna Mkuu wa wa Mamlaka ya Mapato Zanzibar (ZRA) Bw. Yusuph Mwenda wakati wa hafla ya chakula cha jioni Shirika la Maendeleo la Ujerumani (GIZ) jijini Dodoma leo Novemba 16, 2023.

==============================================================

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Maganga amesema kuwa uhusiano kati ya Tanzania na Ujerumani ni wa mfano kwani umeleta manufaa makubwa nchini.

Amesema hayo wakati wa hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na Shirika la Maendeleo la Ujerumani (GIZ) Novemba 16, 2023 jijini Dodoma.

Bi. Maganga amesema kuwa kwa zaidi ya miaka 60 ya uhusiano baina ya nchi hizo mbili umezidi kuimarika kutokana na diplomasia iliyojengwa na viongozi wa nchi yetu kwa muda mrefu.

Amesema uhusiano huo umekuwa chachu ya ziara ya Rais wa Ujerumani Mhe. Frank-Walter Steinmeier aliyefanya ziara ya kikazi nchini Tanzania wiki mbili zilizopita.

Ameishukuru Serikali ya Ujerumani kwa kushirikiana na Tanzania katika sekta mbalimbali kupitia miradi ikiwemo ya mabadiliko ya tabianchi na upatikanaji wa maji akisema kuwa hiyo ni ajenda ya kidunia hivyo ni muhimu kukabiliana na athari zake.

Hali kadhalika ametoa shukrani na pongezi kwa Serikali ya Ujerumani kupitia GIZ Tanzania inavyoshiriki katika kukabiliana na ukatili wa kijinsia ambao ni changamoto inayogusa baadhi ya maeneo nchini.  

Kwa upande wake Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Mhe. Thomas Terstegen ameshukuru na kutoa pongezi kwa Waheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na Rais Frank-Walter Steinmeier ambao wamefungua milango zaidi ya diplomasia kati ya nchi hizo mbili.

Amesema kuwa miongoni mwa mambo aliyohimiza Rais Steinmeier wakati wa ziara yake nchini, ni wananchi kuchangamkia fursa za kiuchumi zinazopatikana ndani ya ushirikiano baina ya nchi hizo mbili. 

Balozi huyo pia, amesema ni matumaini kuwa Ujerumani na Tanzania zitaendeleza ushirikiano wao ambao umedumu kwa zadi ya miaka 60.

Hafla hiyo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali kutoka Tanzania Bara na Zanziba wakiwemo baadhi ya Makatibu Wakuu na wadau kutoka mataifa mbalimbali.

By admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *