Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Maganga akifungua Warsha ya Mafunzo ya Kikanda kuhusu Mpango wa Matumizi ya Eneo la Bahari na Ukanda wa Pwani ya Magharibi mwa Bahari ya Hindi iliyofanyika Jijini Dar es salaam hivi karibuni ambapo Tanzania ilikuwa mwenyeji wa warsha hiyo inayohusisha wajumbe kutoka nchi 10 wanaotekeleza Mkataba wa Nairobi unaohusu Hifadhi, usimamizi na uendelezaji wa Mazingira ya Bahari na Ukanda wa Pwani ya Magharibi.

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Bi. Mary Maganga akifurahia jambo na wajumbe wa warsha ya Mafunzo ya Kikanda kuhusu Mpango wa Matumizi ya Eneo la Bahari na Ukanda wa Pwani ya Magharibi mwa Bahari ya Hindi iliyofanyika Jijini Dar es salaam hivi karibuni ambapo Tanzania ilikuwa mwenyeji wa warsha hiyo inayohusisha wajumbe kutoka nchi 10 wanaotekeleza Mkataba wa Nairobi unaohusu Hifadhi, usimamizi na uendelezaji wa Mazingira ya Bahari na Ukanda wa Pwani ya Magharibi.

Katibu Mkuu Wizara ya Uvuvi na Uchumi wa Bluu, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dkt. Abooud Jumbe akizungumza jambo wakati wa ufunguzi wa warsha ya Mafunzo ya Kikanda kuhusu Mpango wa Matumizi ya Eneo la Bahari na Ukanda wa Pwani ya Magharibi mwa Bahari ya Hindi iliyofanyika Jijini Dar es salaam hivi karibuni huku Tanzania ikiwa mwenyeji wa warsha hiyo inayohusisha wajumbe kutoka nchi 10 wanaotekeleza Mkataba wa Nairobi unaohusu Hifadhi, usimamizi na uendelezaji wa Mazingira ya Bahari na Ukanda wa Pwani ya Magharibi.

Wajumbe wa warsha ya Mafunzo ya Kikanda kuhusu Mpango wa Matumizi ya Eneo la Bahari na Ukanda wa Pwani ya Magharibi mwa Bahari ya Hindi iliyofanyika wakifuatilia mada mbalimbali zilizowasilishwa wakati wa warsha hiyo iliyofanyika Jijini Dar es Salaa hivi karibuni, Tanzania ikiwa mwenyeji wa warsha hiyo inayohusisha wajumbe kutoka nchi 10 wanaotekeleza Mkataba wa Nairobi unaohusu Hifadhi, usimamizi na uendelezaji wa Mazingira ya Bahari na Ukanda wa Pwani ya Magharibi.

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Maganga akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa warsha warsha ya Mafunzo ya Kikanda kuhusu Mpango wa Matumizi ya Eneo la Bahari na Ukanda wa Pwani ya Magharibi mwa Bahari ya Hindi iliyofanyika Jijini Dar es salaam, tarehe 7 Novemba 2022. Tanzania ilikuwa mwenyeji wa warsha hiyo inayohusisha wajumbe kutoka nchi 10 wanaotekeleza Mkataba wa Nairobi unaohusu Hifadhi, usimamizi na uendelezaji wa Mazingira ya Bahari na Ukanda wa Pwani ya Magharibi.

=================================================================

Serikali imesema itaendelea kuimarisha sera, mipango na mikakati ya usimamizi wa rasilimali za bahari na kuongeza wigo wa manufaa ya kijamii na kiuchumi baina ya nchi wanachama zinazotekeleza Mkataba wa Nairobi.
Rai hiyo imetolewa hivi karibuni Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Maganga wakati akifungua Warsha ya Kikanda kuhusu Mpango wa Matumizi ya Eneo la Bahari na Ukanda wa Pwani ya Magharibi mwa Bahari ya Hindi iliyoshiriki nchi 10 zinazotekeleza Mkataba wa Nairobi unaohusu Hifadhi, usimamizi na uendelezaji wa Mazingira ya Bahari na Ukanda wa Pwani ya Magharibi.
Maganga amesema lengo la warsha hiyo ni kujenga uwezo wa wataalamu kutoka nchi wanachama wa Mkataba wa Nairobi katika kuandaa na kutekeleza Mpango wa Matumizi ya eneo la Bahari, Usimamizi wa taarifa za kimazingira, kubadilishana uzoefu na kufahamu hatua zilizofikiwa na nchi wanachama katika kuandaa na kutekeleza mpango wa Matumizi ya eneo la Bahari.
Amesema warsha hiyo itasaidia kuandaa mpango na usimamizi endelevu wa matumizi ya rasilimali za bahari ikiwa ni pamoja na mgawanyo sahihi wa matumizi ya bahari na kuongeza kuwa Tanzania imejipanga kikamilifu ambapo imendaa mpango huo kwa kuzingatia kuwa uchumi wa bluu kuwa ni miongoni mwa agenda za dunia.
Ninapozungumzia uchumi wa bluu ninasisitiza usimamizi endelevu na shirikishi wa mifumo ikolojia ya Pwani na bahari ya Tanzania ili kuendelea kutoa bidhaa na huduma muhimu ikiwa ni pamoja masuala ya uvuvi na uchimbaji wa mafuta na gesi pale vitakakapogundulika,” amesema Bi. Maganga.
Akifafanua zaidi amezitaja nchi zinazotekeleza Mkataba wa Nairobi kuwa ni pamoja na Tanzania, Comoro, Kenya, Somalia, Madagascar, Mauritius, Msumbiji, Shelisheli, Re-Union na Afrika Kusini ambapo kupitia warsha hiyo wataalamu wa mataifa hayo watajadili ajenda mbalimbali za mazingira na jitihada zinazopaswa kuchukuliwa na nchi wanachama.
Kwa upande wake, Mratibu kutoka sekretarieti ya Mkataba huo, Bw. Dixon Waruinge amesema nchi wanachama wa Mkataba wa Nairobi hazina budi kuwa na mkakati wa pamoja wa usimamizi na uhifadhi wa rasilimali za bahari katika katika ukanda ya bahari ya Hindi kwa kuwa ni moja ya hatua muhimu ya kukabiliana na majanga mbalimbali ikiwemo mabadiliko ya tabia nchi.
“Sote ni mashahidi kwa kile kilichotokea kwa nchi za Msumbiji, Malawi na Madagascar ambazo zilikabiliwa na kimbunga cha Freddy ambacho kilileta madhara mbalimbali ikiwemo vifo vya binadanu na viumbe hai wengineJuhudi za pamoja ni muhimu katika kuimarisha hifadhi za bahari amesema Waruinge
Nae wakilishi wa Shirika la Kimataifa la Uhifadhi wa Mazingira Asili ya Dunia (IUCN) Bi. Minna Epps amesema jitihada za pamoja baina ya wadau wa mazingira bado zinahitaji katika kuhakikisha nchi zote zinaendelea kuweka mkazo katika uhifadhi na usimamizi endelevu wa rasilimali za bahari kuokoa uhai wa rasilimali zilizopo.

By admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *